JENNIFER KYAKA(ODAMA)

  • Jennifer Kyaka (Odama) ni mwigizaji, producer wa filamu nchini Tanzania na ni mkurugenzi wa kampuni ya J-Film 4 Life iliyoko Biafra Kinondoni Dar es Salaam.

  • Jennifer Kyaka 'Odama'
  • Jennifer Kyaka a.k.a Odama mzaliwa wa pande za Kagera. Alizaliwa Agositi 8,1983 na shule ya msingi alisoma Kienzya iliyopo Kigoma mjini na baadaye Sekondari ya Minja iliyopo Ugweno, Moshi
  • Mwaka 2006 licheza filamu yeke ya kwanza kwa jina la Shumilleta iliyoandaliwa na Mussa Banzi.
  • Filimu ambazo ameaanda mwenyewe ni Broken Promise, The end of Love na The Avenger.
  • J-Film ni kampuni ya filamu iliyoanzishwa mwaka 2010 ikiwa imedhamiria kutengeneza filamu nchini na nje ya Tanzania kwa viwango vya kimataifa. J-Film 4 Life inazingatia kile mteja anakitaka hasa katika suala la muda (deadline), ubora wa picha (quality) na sauti (sound), vinakuwa katika viwango vya juu.
  • J-Film 4 Life imeweka kipaumbele sana suala la ujumbe unaotolewa na waingizaji kuwa haupotoshi jamii na badala yake unaelimisha, adibisha, fundisha na kumfikia msikilizaji na mtazamaji ipasavyo. Kama Mkurugenzi wa J-Film 4 Life, ninapenda sana kufanya kazi na wasanii wa aina yoyote na mahali popote.