JINSI YA KUPATA PESA KUTUMIA FACEBOOK YAKO>>>>>>
Facebook inaweza kuwa njia ya kuamika ya kupata mapato ya ziada. Unaweza kupata Pesa kwa kufanya mambo yafuatayo
1. Tengeneza page kisha tupia habari zinazovutia watu ,Page ikiwa na Like nyingi kuanzia Like 10000 na kuendelea uza .Page ya LIKE 10000 unaweza kuiuza kwa Tsh 50000 hadi 100000
2.Kutangaza bidhaa za watu/makampuni: Kupitia mtandao mkubwa utakaoweza kujenga kwa kutumia internet, utaweza kutangaza bidhaa za watu au asasi mbalimbali. Mfano waweza tangaza bidhaa za watu kupitia blogu yako(yenye wasomaji wengi), au kupitia ukurasa wako wa Facebook, au kupitia huduma maalum ya kutangaza kwa barua pepe, ambapo utawaomba watu wajiandikishe kupata updates mbalimbali ikiwemo matangazo ya ofa mbalimbali za bidhaa. Waweza pia tangaza bidhaa kwa website/blogu yako kwa kupitia Affiliate programs, ambapo utalipwa kuendana na ‘clicks’ zitakazoingiza wateja kwa asasi fulani.
3.Kutangaza bidhaa zako: Kuna njia nyingi za kutangaza bidhaa zako kupitia internet, kuanzia kutangaza bure au hata kulipia matangazo yako. Waweza kutumia akaunti yako ya Facebook au GooglePlus kutangaza bidhaa zako. Waweza tengeneza blogu na kupitia blogu hiyo ukaweka matangazo yako. Au ukaamua kulipia matangazo kwa blogu za watu wengine, ukatangaza kupitia Facebook, na website mbalimbali