ROSE NDAUKA AJIPANGA KUFANYA MAKUBWA MWAKA HUU
Msanii nyota kwenye tasnia ya filamu Rose Ndauka amefunguka masuala mbalimbali yahusuyo tasnia hiyo, na kuzungumzia ujio wake mpya baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu, jambo lililopelekea mashabiki wake kuhoji kwanini ameamua kukaa kimya muda wote huo?
Akizungumzia ukimya wake Rose Ndauka ameeleza kuwa alikuwa anajipanga zadi ili akija kurudi aje kwakishindo kikubwa, na kueleza kuwa amejipanga kuja na Magazine yake ya Rozie Magazine ambayo atatoa nakala zake, tofauti na awali ambapo ilikuwa inapatikana kwenye mtandao tu (Online).
Licha ya kuja na Magazine Rose Ndauka ameeleza kuwa kwa sasa anamiliki wasanii wa Filamu na Bongo Fleva ambao tayari wamekwisha fanya kazi ambazo anaimani zitawakata kiu mashabiki wake, baada ya kimya cha muda mrefu.