HARARE, Jeshi la polisi nchini Zimbabwe wametangaza kuyapiga marufuku maandamano ya aina yoyote nchini humo

HARARE, Jeshi la polisi nchini Zimbabwe wametangaza kuyapiga marufuku maandamano ya aina yoyote nchini humo. Tangazo hili limetolewa kupitia taarifa maalum iliyotolewa na jeshi hilo na kusambazwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari nchini humo.
Polisi imechukua hatua hizo ikiwa ni siku chache baada ya kutokea maadamano ya wanaompinga rais wa nchi hiyo Robert Mugabe. Huku wazee wastaafu wanaoipinga serikali ya rais huyo nao wakijiandaa kuingia barabarani kuupinga utawala huo.
Mkuu wa polisi jijini Harare Newbert Saunyama,  amekaririwa akisema:
“Marufuku hiyo imepigwa kwa maandamano ya aina zote kwa muda wa mwezi mmoja, kuanzia Ijumaa ya wiki iliyopita.