KAMA UNAKULA NGURUWE HABARI HII ISIKUPITE,Hofu juu ya nguruwe wanaodungwa sindano za homoni Madagascar
Je ni hatari kula nguruwe? Hilo ndilo swali wanalojiuliza watu wa Madagascar baada ya utata juu ya kuwepo kwa vichocheo (homoni) hatari kwenye nyama za nguruwe.
Baadhi ya wakulima nchini humo wamekuwa wakitumia dawa zinazoitwa Confiance, ambazo kwa kawaida ni vichocheo vya mwili (homoni) ambavyo huingizwa mwilini mwa mwanamke kwa njia ya sindano kwa ajili ya kupanga uzazi, ili kuwanenepesha nguruwe.
Mwaka jana, serikali ilipiga marufuku mauzo ya kiholela ya dawa za vichocheo vya mwili , baada ya uchunguzi kufichua kwamba 87% ya nguruwe wanaouzwa sokoni wanavichocheo vya mwili vinavyotumiwa kwa ajili ya kuzuia mimba.
Maafisa nchini Madagascar wameiambia BBC kuwa wanaanzisha uchunguzi kuhusu madhara ya afya ya biadamu yanayoweza kusababishwa na dawa hizo, ambazo zimekuwa zikitumiwa tangu mwaka 2010.
Vinapotumiwa kama tiba, sindano ya vichocheo hivyo vya mwili inaweza kusababisha athari kama vile kuongezeka kwa unene, ukosefu wa raha, kuchoka kwa mwili na hufanya mifupa ya mwili kuwa dhaifu, lakini haijabainika ikiwa ulaji wa chakula chene dawa hizo unasababishahatari zozote.