KUPATWA KWA JUA RUJEWA ,ANGALIA TUKIO ZIMA HAPA
LEO Septemba Mosi, watalii na wanaanga kutoka mataifa mbalimbali duniani wakiwemo wanafunzi wa shule wameungana kushuhudia tukio kubwa na la kihistoria la kupatwa kwa jua katika Kata ya Rujewa wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.
Ikumbukwe kuwa tukio kama hilo la kupatwa kwa jua lilitokea Julai 31,1962 takribani miaka 50 iliyopita na tukio lingine lilitokea Aprili 18, 1977, na wataalamu wa anga wanabainisha kuwa tukio kama hilo litatokea tena hapa nchini Mei 21, 2031.
Tukio hili la kupatwa kwa jua katika eneo hilo la Kata ya Rujewa litatokea leo kuanzia majira ya saa 4:17 asubuhi ambapo eneo hilo litaonekana kwa asilimia 90 hadi umbali wa kipenyo cha kilometa 100.
Serikali ya Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya ambayo itakuwa mwenyeji katika kushudia tukio kubwa na la kihistoria la kupatwa kwa jua, imewahakikishia ulinzi na usalama wa kutosha wageni wote watakaojumuika leo kushuhudia tukio hilo.