Maajabu duniani Azifukua Maiti na Kuzivika Suti Mpya
INDONESIA: Kabila la Torajan la nchini Indonesia wamefukua maiti za ndugu zao kwenye makaburi na kuzivika nguo mpya.
Tukio hilo hufanyika kila baada ya miaka mitatu ambapo hufukua maiti na kuzivika nguo mpya ikiwa ni pamoja na kubadili majeneza ya zamani na kuweka mapya.
Maiti baada ya kufukiliwa na kuvalishwa suti mpya.
Ndugu wakionesha maiti iliyovikwa suti na nyingine ambayo haijavikwa suti.
Maiti baada ya kuvikwa nguo tayari kurudishwa kaburini.
Ndugu wakipiga picha na maiti.
Picha ya maiti iliyopigwa akiwa hai na baada ya kufukuliwa.
Baada ya kuzivika nguo hizo tukio la kupiga picha za kumbukumbu hufuata na baada ya tukio hilo maiti hizo hurudishwa kwenye makaburi yao na kufukiwa tena.
Tamasha hilo hujulikana kwa jina la Ma’nene.