MAN FONGO ATAJA MAFANIKIO MAKUBWA ALIYOYAPATA KUTOKANA NA MUZIKI WA SINGELI


Msanii wa muziki wa Singeli nchini Man Fongo amefunguka na kusema anashangaa mafanikio makubwa ambayo ameyapata ndani ya muda mfupi kupitia muziki wa Singeli hususani kupitia kazi yake ya ‘Hainaga ushemeji’ ambayo imemtambulisha vyema kwa jamii.

Man Fongo kupitia kipindi cha Planet Bongo ya EATV alisema kuwa muziki huo umebadilisha maisha yake ndani ya muda mfupi na sasa anaona maisha kwake ni kama mepesi akilinganisha na kipindi cha nyuma.

“Kupitia Singeli saizi nimepanga nyumba nzima Tabata, nina miliki gari yangu Toyota Altezza , unajua haya kwangu ni mafanikio yaliyokuja kwa muda mfupi sana kutoka kuishi gheto chumba kimoja mpaka sasa naishi nyumba nzima, familia saizi inaniangalia mimi hivyo naweza kusema Singeli ina neema sana kwangu na mafanikio kwangu yamekuja haraka mpaka nashangaa” alisema Man Fongo

eatv.tv