RIPOTI KAMILI YA MATOKEO YA DARASA SABA (7) MWAKA 2016, WANAFUNZI NA SHULE BORA KITAIFA



Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kupitia Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) jana October limetangaza matokeo ya mtihani wa Darasa la Saba huku ikionesha kuwa UFAULU umepanda kwa asilimia 2.52 kutoka asilimia 67.84 mwaka jana hadi asilimia 70.36, huku wavulana waking’ara katika matokeo hayo ambao wengi wametoka shule za Kanda ya Ziwa.

Aidha, watahiniwa 238 kutoka shule sita wamefutiwa matokeo yao baada ya kubainika wamefanya udanganyifu katika mtihani huo.

Akitangaza matokeo hayo Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), Dk Charles Msonde alisema kati ya wanafunzi 10 bora waliofanya vizuri katika mtihani huo, msichana ni mmoja tu, Justina Gerald wa Shule ya Msingi ya Tusiime ya jijini Dar es Salaam.

WANAFUNZI 10 BORA KITAIFA: Ni Japhet Stephano, Jamal Athuman na Enock Bundala (Kwema), Justina na Shabani Mavunde (Tusiime), Jacob Wagine, Isaac Isaac, Daniel Kitundu na Benjamin Benevenuto (Kwema) na Azad Ayatullah (Kaizirege).

WASICHANA 10 BORA KITAIFA: ni Justina na Danielle Onditi (Tusiime), Linda Mtapima (Kaizirege), Cecilia Kenene (Mugini), Magdalena Deogratias (Rocken Hill), Asnath Lemanya (Tusiime), Fatuma Singili (Rocken Hill), Ashura Makoba (Kaizirege), Rachel Ntitu (Fountain of Joy) na Irene Mwijage (Atlas).

WAVULANA 10 BORA KITAIFA: Ni Japhet Stephano, Jamal Athuman na Enock Bundala (Kwema), Shabani Mavunde (Tusiime), Jacob Wagine, Isaac Isaac, Daniel Kitundu na Benjamin Benevenuto (Kwema), Azad Ayatullah (Kaizirege) na Benezeth Hango (Kwema).

SHULE 10 BORA KITAIFA: Ni Kwema na Rocken Hill (Shinyanga), Mugini (Mwanza), Fountain of Joy na Tusiime (Dar es Salaam), Mudio Islamic (Kilimanjaro), Atlas (Dar), St Achileus (Kagera), Giftskillfull (Dar) na Carmel (Morogoro).

SHULE 10 ZILIZOFANYA VIBAYA: Ni Mgata, Kitengu, Lumba Chini (Morogoro), Zege na Kikole (Tanga), Magunga ya Morogoro, Nchinila ya Manyara, Mwabalebi (Simiyu) Ilorienito (Arusha) na Chohero ya Morogoro.

MIKOA 10 ILIYOONGOZA KITAIFA: Ni Geita, Katavi, Iringa, Dar es Salaam, Kagera, Mwanza, Kilimanjaro, Arusha, Njombe na Tabora.

HALMASHAURI 10 BORA KITAIFA: Ni Mpanda Manispaa, Geita Mji, Arusha Mji, Mafinga Mji, Chato, Mwanza Jiji, Moshi Mji, Mji Makambako, Ilemela na Hai.