BARAKA The Prince Aikana TIMU KIBA , ASEMA DIAMOND NI ROLE MODEL WAKE
Kama ulijua Barakah The Prince ni team Kiba, utakuwa umekosea kwa mujibu wa muimbaji huyo.
Hitmaker huyo wa Nisamehe adai kuwa hayupo team yoyote kati ya Kiba na Diamond ila anachotaka yeye ni mashabiki kutoka pande zote hizo mbili.
“Mimi sina team kiukweli. Mimi ni shabiki wa Diamond lakini pia ni shabiki wa Ali. Diamond ameleta heshima kubwa kwenye muziki wa Bongo Fleva. Ali ni msanii mkongwe ambaye ameniispire sana kuingia kwenye huu muziki, lakini pia Diamond anafaa kuwa role model. Mimi nataka mashabiki wa team zote,” amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio.
Muimbaji huyo yupo chini ya kampuni ya Rockastar4000 inayo msimamia Alikiba na Lady Jaydee.