SHILOLE AWAPA MAKAVU WANAOMCHUKULIA POA, ASEMA YEYE NI SHUJAA NA MPAMBANAJI.

Nikijiangalia nilipotoka najikuta najikubali vibaya mno, katika mashujaa nathubutu kujiita mimi SHUJAA!! Nimetokea kwenye familia ya chini, na huenda hata kwenye familia yangu hakuna alietegemea mimi kufika nitapofika kwa jinsi hali yetu ilivyokuwa, nimekuja mjini hakuna niliekuwa namjua, nimewakuta watu mjini hapa na NIMEWAACHA!!! Nimepitia mengi sana, nimedharauliwa na wengi mno, wakati naanza kuimba watu wengi walinicheka na kuniona sina ninachojua, lakini leo huyu hapa waliocheka wengi leo wananiangalia kwa mbali, kupitia filamu na muziki kuna watu walinidharau na kuniletea USTAR lakini mimi leo star zaidi yao, na wao naona bado wanapigwa na jua tu!! Hapo ndio ujue haya maisha tu, usifike sehemu ukajiona kama vitu vitabaki vilivyo milele, mambo yanaenda yanabadilika kila siku

Lakini zaidi tusichukuliane poa, hatujafika tulipofika kimchezomchezo, nimepitia mengi mno, usinione jukwaani pale ukataka kunichukulia poa, nimestruggle kufika nilipofika, NIMEPAMBANA!!! Na kuna watu kibao wanaofaidika kwasasa kupitia hikihiki ninachokifanya, na bado hakuna kukata tamaa..
zaidi mjue mi kwangu huu mwanzo tu ila nawaahidi NITAENDELEA KUWASURPRISE mpaka mjiulize nimefikaje nilipofika, msichojua siri ni moja tu KUPAMBANA!!! Popote ulipo Pambana tu, milango iko mingi ya kutokea inakusubiri wewe kuamua.