Idara ya Uhamiaji yatangaza nafasi za kazi

Idara ya Uhamiaji yatangaza nafasi za kazi

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Kamishna Mkuu wa Uhamiaji anatangaza nafasi za kazi katika Idara ya Uhamiaji. Nafasi hizo ni Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji, Koplo wa Uhamiaji na Konstebo wa Uhamiaji.

A.      MKAGUZI MSAIDIZI WA UHAMIAJI (Nafasi 70)
         
  • SIFA ZINAZOHITAJIKA
  • Awe na Shahada ya Kwanza au Stashahada ya Juu kutoka Vyuo Vikuu vinavyotambuliwa  na Serikali katika fani zifuatazo:
Sheria, Uchumi, Biashara, Utawala, Uandishi wa Habari, Ualimu, Usafirishaji, Raslimali Watu, Sayansi ya Kompyuta, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Takwimu, Uchapaji, Uhandisi Majengo na Uhandisi Mitambo.
  • Awe na umri usiozidi miaka 35
  • MAJUKUMU NA KAZI ZA KUFANYA
  • Kusimamia doria sehemu za Mipakani, Bandarini, Vituo vya Mabasi, Treni na sehemu zenye vipenyo vya kuingia na kutoka nchini vikiwemo vya majini
  • Kusimamia shughuli za upelelezi, kuandaa Hati ya Mashitaka na kuendesha mashitaka
  • Kutoa na kupokea fomu mbali mbali za maombi ya Hati za Uhamiaji
  •     Kufanya Ukaguzi wa Mwanzo wa Maombi mbalimbali
  • Kuagiza ufunguaji wa Majalada ya watumiaji
  •  Kupokea na kukagua Hati za Safari, Fomu za Kuingia na Kutoka Nchini
  • Kuidhinisha malipo mbalimbali ya huduma za Uhamiaji kwa wanaostahili
  • Kutunza kumbukumbu za ruhusa za watu wanaoingia na kutoka nchini
  • Kukusanya, kusimamia na kutunza takwimu za Uhamiaji na Uraia
  • Kuandaa majibu ya maombi yote ya huduma za uhamiaji yaliyokubaliwa au kukataliwa

B:      KOPLO WA UHAMIAJI (Nafasi 100)      
1.      SIFA ZINAZOHITAJIKA:
  • Awe amehitimu Kidato cha Sita na kufaulu
  • Awe na umri usiozidi miaka 30
C.      KONSTEBO WA UHAMIAJI (Nafasi 100)
1.      SIFA ZINAZOHITAJIKA:
  • Awe amehitimu Kidato cha Nne na kufaulu
  • Awe na umri usiozidi miaka 25
D:      SIFA ZA ZIADA: KOPLO/KONSTEBO WA UHAMIAJI
  • Cheti cha Ufundi Stadi (Full Technical Certificate) kwenye fani ya Umeme na Mitambo
  • Cheti au Stashahada ya Uhaziri (Certificate or Diploma in Secretarial Studies) kutoka Chuo kinachotambulika na Serikali
  • Cheti au Stashahada ya Kutunza Kumbukumbu (Certificate in Records Management) kutoka Chuo kinachotambulika na Serikali
  • Cheti au Stashahada ya Takwimu (Certificate or Diploma in Statatistics ) Kutoka Chuo kinachotambulika na Serikali.
  • Cheti au Stashahada ya Vyombo vya Majini (Certificate or Diploma in Marine Transportation and Operations) kutoka Chuo kinachotambulika na Serikali
  • Cheti au Stashahada katika fani ya Uchapaji (Printing)
  • Ujuzi na Elimu ya Kompyuta na Uandishi mzuri utazingatiwa
  • Cheti cha Ufundi Makanika,Kozi ya juu ya Udereva na Leseni ya Udereva Daraja C
E.       MAJUKUMU NA KAZI ZA KUFANYA
  •  Kufungua, kupanga na kutunza majalada ya huduma mbalimbali za Uhamiaji
  •      Kuandika Hati mbalimbali za Uhamiaji
  • Kufanya doria sehemu za Mipakani, Bandarini, Vituo vya Mabasi, Treni na sehemu zenye vipenyo vya kuingia na kutoka nchini vikiwemo vya majini.
  • Kusindikiza watuhumiwa wa kesi za Uhamiaji Mahakamani pamoja na wageni wanaofukuzwa nchini
  • Kufanya ukaguzi kwenye mahoteli, nyumba za kulala wageni na sehemu za biashara.
  • Kuchapa au kuandika kwa kompyuta barua au nyaraka mbalimbali zinazohusu kazi za kila siku za Uhamiaji.
  • Kufanya matengenezo/ukarabati wa mitambo na vitendea kazi vya Uhamiaji
  • Kuandaa na kutunza takwimu za huduma mbalimbali za uhamiaji
F.       MAOMBI YOTE YAWE NA VIAMBATISHO VIFUATAVYO:
  • Nakala za vyeti vya kuhitimu masomo kwa mujibu wa sifa zilizotajwa
  • Nakala ya Cheti cha Kumaliza Elimu ya Msingi
  • Nakala ya Cheti cha Kuzaliwa
  • Picha mbili (Passport Size)
  • Barua ya Utambulisho kutoka kwa Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa
G.      UTARATIBU WA KUTUMA MAOMBI
Maombi yote yapitie posta na barua za maombi ziandikwe kwa mkono.
  • Maombi ya nafasi ya Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji yatumwe kwa:
KATIBU MKUU,
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI,
S.L.P. 9223,
DAR ES SALAAM
  • Maombi ya nafasi ya Koplo wa Uhamiaji na Konstebo wa Uhamiaji yatumwe kwa:
KAMISHNA MKUU WA UHAMIAJI,
S.L.P. 512,
DAR ES SALAAM
         
Mwisho wa kutuma maombi kwa nafasi zote ni tarehe 27/02/2014
Chanzo: Tovuti ya Immigration ;