BAADA YA SOKO LA FILAMU KUBADILIKA ,MKONGWE WA FILAMU SALOME URASSA"THEA" KACHUKUA MAAMUZI MAGUMU..........

Msanii mkongwe wa filamu, Salome Urassa ‘Thea’ amesema anajipanga kuachia tamthilia 3 mpya baada ya soko la filamu kudai kubadilika.
Akiongea na Bongo5 Jumapili hii, Thea amesema kuongezeka kwa runinga kumewafanya wasanii wa filamu kufikiria nje ya box kwa kutengeza tamthilia.
“Kusema kweli sasa hivi tamthilia za kwenye runinga ndo zimekuwa issue, runinga nyingi zinahitaji bidhaa hiyo, kwa hiyo wasanii wengi baada ya kuona hiyo fursa tukaichangamkia, kama mimi tayari na tamthilia tatu ambazo zikikamika zitaanza kuonyeshwa kwenye runinga,” alisema Thea.
Aliongeza, “Unajua tamthiria unaweza kuiuza zaidi ya runinga moja, kwa hiyo mimi binafsi naona ni biashara nzuri ambayo kama tukiikazania soko letu la filamu litakuwa sana,”
Pia muigizaji huyo amesema ataendelea kutoa filamu za kawaida kwa kuwa huko ndiko kuliko mlea.