BREAKING NEWS!!!!!!!!!! TAARIFA YA KUSIKITISHA, Tundu Lissu HAJULIKANI ALIPO NI BAADA YA JANA KUKAMATWA NA POLISI SINGIDA


Baada ya kukamatwa jana jioni kisha kusafirishwa jana hiyo hiyo kuelekea jijini Dar es Salaam kwa kadri ya kile kilichodaiwa kuwa ni maagizo kutoka juu, walipofika Dodoma baada ya kula na kupelekwa polisi mkoa kuonana na RCO ilionekana kuwa yeye pamoja na askari waliokuwa wakimsindikiza wangelala pale na safari ya kupelekwa Dar es Salaam ingeendelea asubuhi leo.



Viongozi wa chama kutoka Singida waliokuwa wakimsindikiza waliambiwa kuwa wanaweza kutafuta mahali pa kulala na kwamba wafike hapo polisi mkoa majira ya saa moja asubuhi leo ambapo safari ingeanza saa mbili.

Taarifa zilizotufikia alfajiri leo kutoka kwa viongozi wa chama mkoani Dodoma na viongozi waliokuwa wakimsindikiza Mwanasheria Mkuu wa Chama na Mbunge huyo wa Singida Mashariki, zinasema kuwa baadhi yao wamefika polisi hapo saa 12 asubuhi na hawakumkuta Lissu bali wameambiwa kuwa ameondolewa hapo mapema alfajiri kwa maelekezo ya kutoka juu.

Haijulikani hasa muda ambao ameondoka Dodoma na kwa sasa atakuwa yuko wapi na iwapo alitokea central police station au Ofisi ya RCO!




Source: Jamii Forum