Kauli ya CHADEMA Kuhusu Hatua za NHC na Rasilimali za Mwenyekiti Mbowe
Kutokana na habari zilizoandikwa leo na vyombo vya habari mbalimbali nchini kuhusu tukio la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kupitia kwa madalali wake 'kuvamia' jengo lenye rasilimali za Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe; Kwa kuwa habari hizo zimehusisha hatua hiyo ya NHC na itikadi au msimamo wa kisiasa wa Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe ambaye ni mmoja wa wanahisa wa Mbowe Hotels Ltd ambayo ni mmiliki wa rasilimali hizo zilizovamiwa (Ofisi za Free Media na Club Billicanas) na waandishi wa habari wametutafuta kutaka kauli ya chama juu ya suala hilo; Katika hatua ya sasa, tunapenda kusema kuwa Chama kitalitolea msimamo suala hilo baada ya kuwasiliana na kushauriana na wanasheria wa Mwenyekiti Mbowe ambao wanalisimamia na kulifanyia kazi suala hilo mahakamani. Imetolewa, Sept' 2, 2016 na;
Tumaini Makene Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano CHADEMA