Mama Lwakatare Awatoa Wafungwa 12 katika Gereza Keko
Kanisa la Assemblies of God, Mikocheni B (Mlima wa Moto) chini ya kiongozi wake, Mchungaji Dk. Getrude Lwakatare, limewatoa wafungwa 12 katika Gereza la Keko lililopo jijini Dar es Salaam.
Zoezi hilo limefanyika leo katika Gereza la Keko na baadaye Dk. Lwakatare ataelekea katika Gereza la Ukonga kwa ajili ya kuendelea na shughuli hiyo.
Akizungumza na wanahabari leo, Mchungaji Lwakatare amesema kuwa amewatoa wafungwa wanaodaiwa kiasi kidogo cha fedha na wenye makosa kidogo ili waweze kurejea uraiani na kujenga taifa kwani kuendelea kuishi huko wanapoteza nguvu kazi ya kesho.
“Waumini wa Kanisa la Mlima wa Moto ndiyo waliochangia kiasi cha shilingi milioni 25 kwa ajili ya kuwatoa jumla ya wafungwa 78 katika awamu ya kwanza, na baadaye kanisa litaendelea na zoezi hilo.” Alisema Mama Lwakatare.