Profesa Lipumba afunguka kuhusu deni la Taifa, ni kila Mtanzania anatakiwa kulipa?
Taarifa zilizochukua headline kwenye magazeti ya leo September 8 2016 ni kuhusu kupanda kwa deni la Taifa ambapo imeelezwa kuwa limepanda kutoka dola za marekani bilioni 19.69 June mwaka jana na kufikia dola 23.2 ambazo ni zaidi ya trilioni 51 sawa na ongezeko la 18%.
Profesa Lipumba akiwa katika kipindi cha power Breakfast cha clouds FM leo September 8 2016 kaelezea jinsi namna deni la Taifa linalipwa na kama ni kila mtanzania anatakiwa kulipa……..
>>>’Deni la taifa ni tofauti na lako wewe mwenyewe, ni kodi ndiyo ambayo itakayolipia deni hilo kwa hiyo kama mmedaiwa sana, mmekopa sana utakuta sehemu kubwa inakwenda kulipia deni badala ya kwenda kutoa huduma‘