Mama wa chura snura mushi asema hana tabia ya Kutoka na Vijana Wadogo
Snura alisema hayo kupitia kipindi cha eNEWZ ya EATV na kudai aliweza kumkiss Raymond wakati anatengeneza video ya wimbo wake ‘Natafuta kiki’ kwani pale alikuwa kazini ila siyo kusema anatoka kimapenzi na msanii huyo kama ambavyo baadhi ya watu walivyoanza kuzusha anatoka naye baada ya kuona picha akimkiss Raymond.
“Baada tu ya kutoka ile picha mimi na RayVany tuki ‘kiss’ watu wakaanza kuniandika vibaya kwenye mitandao ya jamii, sijui RayVany ndiyo mwanaume aliyekuwa anamnyima usingizi Snura jamnii Raymond yule mimi ni mdogo wangu. Nili mkiss pale nilikuwa kazini, kazini naweza kum kiss hata mtoto wangu kama ‘movie’ nayoicheza inaniambia nitembee na mwanangu nitaacha kum kiss? Kwa hiyo pale nilikuwa kazini katika maisha ya kawaida kabisa Raymond mimi ni mdogo wangu, mimi kusema za ukweli huwaga sina tabia za kutoka kimapenzi na wadogo zangu’ alisema Snura.