Matokeo ya mechi zilizochezwa leo Yanga yashindwa kuvunja rekodi yao dhidi ya Ndanda FC Nangwanda, Simba yaua



Ligi Kuu soka Tanzania bara imeendelea leo September 7 kwa michezo mitatu kupigwa katika viwanja vya Taifa Dar es Salaam, Sokoine Mbeya na uwanja wa Nangwanda Sijaona Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara Dar es Salaam Youg Africanswalisafiri wakitokea Dar es Salaam kwenda Mtwara kuwafuata Ndanda FC kwao.



Hata hivyo Yanga ambao walikuwa wanatarajiwa kukutana na upinzania mkubwa kutoka kwa Ndanda FC kutokana na rekodi ya mechi zao za nyuma, Yanga wamelazimishwa suluhu ya 0-0 baada ya Ndanda kufanikiwa kucheza mchezo wakulinda goli lao kwani kipindi cha pili walicheza nyuma zaidi.

Huu ni mchezo wa tano kwa Yanga na Ndanda FC kukutana katika Ligi Kuu sokaTanzania bara, lakini ni mara ya pili kwa timu hizo kucheza katika uwanja wa Nangwandahuku Yanga akiwa kafungwa mara moja katika uwanja huo na kutoa suluhu mara moja, kwa ujumla Yanga na Ndanda wamefungana mara moja moja na kutoka sare mara tatu


Matokeo ya mechi nyingine za VPL zilizochezwa leo September 7


Club ya Simba iliwaalika Ruvu Shooting katika uwanja waUhuru Jijini Dar es salaam ambapo mechi ilimalizika kwa Simba kuibuka na Ushindi wa Magoli 2-1,

Ruvu Shooting ndio ilikua ya kwanza kupata goli katika dakika ya 8 ya mchezo kupitia kwa Abrahaman Musa, wakati magoli ya Simba yalipatikana katika dakika ya 11 kupitia kwa Ibrahim Ajib na dakika ya 50 kupitia kwa Mavugo.
Tanzania Prisons 0-1 Azam F
C