AIKA ATOBOA SIRI YA KUCHOMOKA KIMUZIKI



MSANII ambaye ni mmoja wa wamiliki wa Lebo ya The Industry, Aika Mareale akiwa pia memba wa Kundi la Navy Kenzo, ametoboa siri ya kutoka kwake kisanaa kuwa ni kutojidharau.

Akizungumza na Risasi Vibes, Aika ambao ambaye anaunda kundi hilo akiwa na mpenzi wake, Emmanuel Mkono ‘Nahreel’, akiwa anatamba na kibao chake cha ‘Kamatia Chini’ alisema wakati anaanza muziki hakuwa na matumaini ya kufika alipofikia, lakini hakutaka kujidharau licha ya kazi zake kutosikika.

“Unajua vile zamani unafanya kitu hakisikiki, unahangaika ili muziki wako ufahamike, lakini kamwe sikutaka kujidharau ndiyo maana mpaka sasa nimeweza kuwa mmoja wa mastaa kwenye jamii,” alisema Aika.