Staa wa Filamu za Kibongo na mtangazaji, Lulu Semagongo ‘Aunt Lulu’ Afanya Ufuska Kweupe!
Mtangazaji huyo alikutwa akifanya uchafu kwenye baa moja iliyopo maeneo ya Mbezi-Beach jijini Dar alipokuwa amejumuika na mastaa wa Kundi la Scorpion Girls, Isabela Mpanda, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ na Jacqueline Pentezel ‘Jack wa Chuzi’ ambapo alikuwa akinywa vinywaji vikali na kuvuta sigara. Timu yetu ya Operesheni Fichuo Maovu (OFM) ilimshuhudia Aunt Lulu akiwa amelewa bwii huku akimkatia mauno mwanaume mmoja bila kujali wingi wa watu waliokuwa eneo hilo.
Baada ya kufanikiwa kumrekodi video na kushindwa kuzungumza naye kutokana na hali hiyo ya ulevi, siku iliyofuata mwandishi wetu alimtafuta Aunt Lulu ili kumuhoji sababu ya kujiachia na kutouthamini mwili wake kwa kuvuta sigara na kunywa pombe kali lakini hakupokea simu siku nzima. Gazeti hili linaendelea kumtafuta atakapopatikana atabanwa ili kujua kama kuna kitu kinamsibu hadi aamue kunywa pombe na kuvuta sigara kiasi cha kufanya vitendo vya aibu hadharani.