Waislamu waanza Hija Saudi Arabia,Takriban Mahujaji wa kiislamu milioni 1.5 wamekusanyika nchini Saudi Arabia chini ya ulinzi mkali
Takriban Mahujaji wa kiislamu milioni 1.5 wamekusanyika nchini Saudi Arabia chini ya ulinzi mkali, kabla ya kuanza rasmi ibada ya hija ya kila mwaka.
Magari yamepigwa marufuku ya kukaribia msikiti mkuu, Grand Mosque, ambao ni eneo takatifu zaidi kwa waislamu, huku mahujaji wakifanyiwa ukaguzi na polisi katika vituo kadhaa kwenye eneo hilo.
Zaidi ya mahujaji 2000 waliaga dunia mwaka jana wakati wa ibada ya hija, wengi wao wakiwa raia wa Iran.
Iran iliilaumu Saudi Arabia kwa kutosimamia ibada za Hija inavyofaa, na imekataa kuwaruhusu raia wake kuenda Saudi Arabia kuadhimisha ibada ya Hija.