Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa leo anatarajiwa kuongoza waombolezaji kuaga miili ya watu 16
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa leo anatarajiwa kuongoza waombolezaji kuaga miili ya watu 16 waliopoteza maisha kwenye tetemeko la ardhi lililotokea jana mkoani Kagera.
Zoezi hilo la kuaga miili linafanyika katika Uwanja wa Kaitaba uliopo Bukoba Mjini mkoani Kagera.
Jumla ya watu 16 wamefariki dunia huku zaidi ya 200 wakijeruhiwa.