Yanga yapokea kipigo kizito kutoka kwa Stand United,Pastore Athanasi ndio aliyeiangamiza Yanga

Stand United ‘Chama la Wana’ wamevunja rekodi ya Yanga baada ya kuifunga bao 1-0 kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara uliochezwa uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga.



Bao pekee la Stand limefungwa na Pastore Athanasi ambalo limeifanya tumu take iibuke na pointi tatu kwenye uwanja wa nyumbani.

Licha ya Stand kuwa kwenye mpasuko mkubwa wa kiutawala, timu hiyo bado haijapoteza mchezo wowote hadi sasa tangu kuanza kwa ligi mzimu huu 2016-2017. Imeshinda mechi tatu na kutoka sare kwenye michezo mitatu. (Stand UTD  0-0 Mbao FC, Kagera Sugar 0-0 Stand UTD, Stand UTD 1-0 Toto Africans, Mwadui FC 2-2 Stand UTD, Stand UTD 2-1 Ruvu JKT, Stand UTD 1-0 Yanga)

Rekodi za Yanga zilizovunjwa na Stand United

Stand United imeifunga Yanga kwa mara ya kwanza tangu timu hiyo ya Shinyanga mjini ilipopanda daraja.
Yanga imepoteza mchezo wake wa kwanza wa  VPL msimu baada ya kucheza mechi nne bila kufungwa. Mara ya mwisho Yanga kupoteza mechi ilikuwa 3-1 dhidi ya TP Mazembe nchi DR Congo katika mashindano ya kombe la shirikisho hatua ya makundi.
Stand United imekuwa timu ya kwanza kufunga goli dhidi ya Yanga. Awali Yanga ilikuwa imecheza mechi nne za ligi bila kuruhusu goli huku yenyewe ikiwa imefunga magoli nane. (Yanga 3-0 African Lyon, Ndanda 0-0 Yanga, Yanga 3-0 Maji Maji, Mwadui 0-2 Yanga).
Matokeo ya leo yanaifanya Stand UTD ifikishe jumla ya pointi 12 na kukaa nafasi ya pili nyuma ya Simba SC inayoongoza ligi ikiwa na pointi 16, Yanga inashuka chini kwa nafasi moja hadi nafasi ya tatu ikiwa na pointi 10 baada ya kucheza mechi 5 huku ikiwa na mechi moja mkononi.