Bondia maarufu wa ngumi za kulipwa nchini,Thomas Mashali afariki Dunia

Mwanamasumbwi Thomas Mashali amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana katika eneo la Kimara Jijini Dar es Salaam.
Inadaiwa kuwa wakati bondia huyo alikuwa akinywa pombe na ndipo ulizuka ugomvi na mtu mmoja ambaye anadaiwa kupiga kelele kudai Thomas Mashali ni mwizi.

Kabla ya kufikwa na mauti inadaiwa bondia huyo alikimbizwa katika hospitali ya Sinza Palestina kabla ya kuhamishiwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako aliiaga dunia.