Showing posts with label Michezo. Show all posts

Genk ya Samatta kuwakabili wababe wa Tottenham, Gent katika Europa hatua ya 16-Bora



Genk imepangwa kucheza dhidi ya mahasimu wao wa Ubelgiji Gent hatua ya 16-Bora ambayo si timu rahisi hata kidogo baada ya kuiengua kwenye michuano hiyo Tottehnham Hotspur.

Timu hiyo ya Mbwana Samatta imefika hatua hiyo ya mtoano baada ya kushinda kwa jumla ya mabao 3-2 dhidi ya Astra.

Kadhalika Manchester United nayo imepangwa kuikabili klabu ya Urusi Rostov katika hatua hiyo ya Europa.


Kwa upande mwingine miamba wa Serie A Roma watacheza dhidi ya Lyon ya Ufaransa, huku Schalke ikiikabili Borussia Monchengladbach.

Droo kamili ya Europa hatua ya 16-Bora

Celta Vigo vs Krasnodar

APOEL vs Anderlecht

Schalke vs Borussia Monchengladbach

Lyon vs Roma

Rostov vs Manchester United

Olympiacos vs Besiktas

Gent vs Genk

Kobenhavn vs Ajax

Read More »

YANGA YAFANYA MAUAJI COMORO, YATOA KIPIGO KIZITO DHIDI YA NGAYA DE MBE YA COMORO


Yanga imeanza kwa kasi michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuwafunga wenyeji wao Ngaya de Mbe ya Comoro mabao 5-1


Kikosi cha Yanga kimeanza kwa kasi michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuwafunga wenyeji wao Ngaya de Mbe ya Comoro mabao 5-1.

Kipigo hicho kinaifanya Yanga kuwa na kazi nyepesi katika mchezo wa marudiano ambao utapigwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam Jumamosi ijayo.Wawakilishi hao wa Tanzania katika michuano hiyo mi kubwa Afrika walikwenda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao mawili yaliyofungwa na kiungo Mzambia Justine Zullu na winga Simon Msuva.

Zullu akilifunga bao lake la kwanza tangu atue Yanga dakika ya 43, akimalizia kazi nzuri ya Simon Msuva na wakati mashabiki wa Ngaya de Mbe wakiamini watakwenda mapumziko wakiwa nyuma kwa bao moja Msuva alifunga bao la pili dakika ya 45 kazi nzuri ya Haruna Niyonzima.

Yanga ilirudi kwa kasi kipindi cha pili na iliwachukua dakika 9 kufunga bao la pili mfungaji akiwa Mzambia Obrey Chirwa ambaye alimalizia kazi nzuri ya Msuva.

Dakika ya 65 Amissi Tambwe aliifungia Yanga bao la nne baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Niyonzima na kuwakatisha tamaa wenyeji wao Ngaya.

Ngaya walionekana kuzidi kupambana wakitafuta angalau bao la kufutia machozi na jitihada zao zilizaa matunda dakika ya 66 baada ya Said Anfane kufunga bao zuri akimalizia krosi iliyochongwa kutoka winga ya kushoto mwa lango la Yanga.

Baada ya kufungwa bao hilo Yanga walikuwa juu na kuanza kulisakama lango la Ngaya ambapo dakika ya 73 Thabani Kamusoko alifunga bao la pili baada ya kupokea pasi nzuri ya Juma Mahadhi aliyeingia muda fupi kuchukua nafasi ya Tambwe.

Mchezo huo uliendelea kwa timu zote kushambuliana hasa Yanga ambao alipoteza nafasi mbili za wazi katika dakika za 78 na 80 ambapo Mahadhi alishindwa kutumia na kuzitumia nafasi hizo.

Hadi filimbi ya mwisho Yanga iliibuka na ushindi huo mnono ambao sasa itahitaji nguvu kidogo katika mchezo wa marudiano ili kusonga mbele raundi ya kwanza ya michuano hiyo.

Read More »

Angalia mechi ya SIMBA VS PRISONS Live, bofya kuangalia



Read More »

MAJINA YA WANAFUNZI WALIOFANIKIWA KUPATA MKOPO BAADA YA KUAPPEAL 2016/2017




LIST OF SUCCESSFUL LOAN APPELLANTS 2016/2017

The Higher Education Students’ Loans Board wishes to announce successful loan appellants. To view the list click here.


Details of the loan allocations will be available in their respective institutions by end of 13th February, 2017.

Issued by:

EXECUTIVE DIRECTOR
HIGHER EDUCATION STUDENTS’ LOANS BOARD
11th February, 2017.

Read More »

Lipuli FC yapanda daraja ,sasa kucheza Ligi Kuu


Timu ya Lipuli ya mkoani Iringa imerejea ligi kuu Tanzania bara baada ya kupita miaka 17 tangu iliposhuka dara na mkoa huo kukosa timu ya Ligi ya Vodacom kwa kipindi chote hicho.

Kocha msaidizi wa zamani wa Simba raia wa Uganda Richard Amatre ndiye ameipandisha timu hiyo baada ya kusota nayo kwa miaka mitatu ikiishia katika nafasi za pili na tatu.

Amatre alisema "haikuwa kazi rahisi, lakini jitihada zake na wachezaji wake ndivyo vimewasaidia kupanda na kufuzu ligi hiyo ambayo ndiyo ya kwanza kwa ukubwa Tanzania Bara"

“Nawapongeza sana viongozi wa timu wachezaji na wananchi wote wa mkoa wa Iringa, kwa umoja na ushirikiano wao waliouonyesha hadi kufanikiwa kuipandisha timu ligi kuu, lakini pamoja na kupanda bado tunakazi kubwa lengo ni kuhakikisha tunadumu na kupata mafanikio kwenye ligi ya Vodacom,”amesema Amatre.

Kocha huyo amesema walistaili kupanda msimu kutokana na mapambano waliyopitia hadi kufikia hapo lakini pia ubora wa kikosi chake ambacho kilikuwa na nyota wengi wenye ubnora wa hali ya juu kuzidi timu zote zilizokuwa kwenye kundi lao.

Mganda huyo amesema mia yao ilikuwa nikurejea ligi kuu nakufanya mapindunzi ya soka katika mkoa wao wa Iringa, hivyo wanajipanga ili wasishuke daraja tena.

“Mashabiki wetu waendelee kutusapoti na kamwe hatuwezi kuwaangusha tutajituma kadri ya uwezo wetu ili kuwapa matokeo mazuri kama tulivyokuwa tunafanya huku katika ligi daraja la Kwanza”, alisema Amtri.

Lipuli inaongoza kundi hilo ikiwa na alama 29 huku ikibakiwa na michezo miwili mikononi mwao.

Read More »

Azam FC yatoa kipigo cha pili mfululizo kwa Simba ndani ya mwaka 2017




Siku 15 baada ya wekundu wa Msimbazi Simba kucheza dhidi ya Azam FC katika fainali ya Mapinduzi Cup 2017 January 13 visiwani Zanzibar na Simba kupoteza kwa goli 1-0, goli ambalo lilifungwa na Himid Mao, leo January 28 2017 timu hizo zilikutana tena katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom.

Simba na Azam FC leo wamekutana katika uwanja wa Taifa Dar es salaam katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, ikiwa huu ni mchezo wao wa 18 kwa Simba na Azam FC kukutana katika mechi za Ligi Kuu, Simba ikiwa imeifunga Azam FC mara 8, sare mara 5.

Leo January 28 nahodha wa Azam FC John Bocco anaipatia ushindi Azam FC wa goli 1-0, goli ambalo amelifunga dakika ya 71 kwa shuti kali lililomshinda golikipa wa Simba raia wa Ghana Daniel Agyei, ushindi huo wa Azam FC kwa Simba unakuwa wa 5 katika Ligi Kuu Tanzania bara toka waanze kukutana.

Read More »

Mbwana Samatta Kuendelea Kushindania Namba KRC Genk

Siku 14 zimepita toka mshambuliaji wa KRC Genk Nikolaos Karelis ambaye alikuwa anashindania namba na mtanzania Mbwana Samatta atangazwe kuwa atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha miezi 8 hadi 9 kufuatia jeraha la goti la kushoto alilolipata wakati wa mchezo dhidi ya KAA Gent dakika ya 51 December 27.

January 10 2017 KRC Genk imetangaza kukamilisha usajili wa mshambuliaji Jose Naranjo kutokea Celta Vigo ya Hispania, hiyo itakuwa ni changamoto mpya kwa Mbwana Samatta kuendelea kupambania namba ya kucheza na Naranjo katika kipindi ambacho Karelis atakuwa nje.

Jose Naranjo amejiunga na KRC Genk ya Ubelgiji akitokea Celta Vigo ya Hispania kwa mkataba wa miaka mitatu na nusu, Naranjo mwenye umri wa miaka 22 amewahi kuichezea Villarreal kwa mkopo mwaka 2014 akitokea Recreativo.

Read More »

Simba yaiua Yanga kwa 4G , sasa Kucheza Fainali na Azam



Read More »

Uchambuzi : Haji Manara Asema Goli la Henrikh Mkhitaryan ni bora Zaidi kuliko la Olivier Giroud

hajismanaraTumekaa Jopo la Watu Wenye Uweledi wa Kuchambua Kabumbu kwa Kiwango cha HD Tumegundua Goli Alilofunga Giroud Jana Sio "Scorpion Kick", Lile Goli Linaitwa " Ng'ombe Kick"...The Real Scorpion Kick Goal Lilifungwa na Mtaalam Henrikh Mkhitaryan Mwanzoni mwa Juma Lililopita Manchester United Wakiibanjua Sunderland 3-1 Old Trafford.

Kwanini Tunasema Goli la Giroud sio Scorpion Kick Bali Ni Ng'ombe Kick?
Tumeangalia Vitu vingi, Kikubwa kabisa ni Umbile lenyewe la Mdudu Scorpion...Hakuna Scorpion Yoyote amewahi kuoneka akigeuza kichwa chake nyuma na Hakuna Scorpion Yoyote Duniani Amewahi kuonekana akikunja Mkono Wake mmoja kuelekea nyuma na Mmoja kuelekea mbele, Mikono yote ya Scorpion Huielekeza Mbele pamoja na kichwa chake Huwa kina focus mbele halafu Ule mkia Hufanya Kazi ya "Ku-bite" kama akihisi mushkeli yoyote...Angalia kichwa na mikono ya Mikhitaryan unapata Umbile halisia la Mdudu Scorpion, na Angalia kichwa na mikono ya Giroud Utagundua yule ni Ng'ombe Kasimama na Kuamua kurusha Teke Huko Nyuma Litakalompata Atajiju.

Hivyo Basi, Mnaolinganisha Haya Magoli Mawili Mkae Mkijua mnachokifanya ni Kufananisha Kifo na Usingizi...Huwezi kufananisha "Ng'ombe Kick" na "Scorpion Kick" Hata Siku Moja Utachekwa...SCORPION KICK LITABAKI KUWA GOLI BORA KUWAHI KUFUNGWA NA WACHEZAJI BORA PEKEE KATIKA HISTORIA YA MPIRA WA MIGUU.

Read More »

Simba ya washa moto Kombe la Mapinduzi,yaanza kwa kishindo


Baada ya kuchezwa mchezo wa pili wa Kundi wa Kombe la Mapinduzi 2017 leo January 1, usiku wa January 1 ilikuwa ni zamu ya wekundu wa Msimbazi Simba kucheza mchezo wao wa kwanza wa Kundi A dhidi ya Taifa Jang’ombe katika uwanja wa Amaan Zanzibar.

Huu ulikuwa ni mchezo wa kwanza kwa Simba lakini ulikuwa ni mchezo wa pili kwa Taifa Jang’ombe ambao mchezo wao wa awali walicheza dhidi ya Jang’ombe Boys na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0, goli ambalo lilifungwa na Hassan Seif.

Taifa Jang’ombe leo wamekubali kupoteza mchezo dhidi ya Simba kwa goli 2-1, magoli ya Simba yakifungwa na Mzamiru Yassin dakika ya 28 na Juma Luzio dakika ya 42, lakini beki wa Simba Novaty Lufungo akijifunga dakika ya 76 baada ya Taifa Jang’ombe kupiga kona iliyosababisha goli hilo.

Msimamo wa Kundi A utakuwa unaongozwa na URA wenye point tatu na magoli mawili wakifuatiwa na Simba wenye point tatu sawa Taifa Jang’ombe aliyepo nafasi ya tatu kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa, Simba watarudi uwanjani January 3 kucheza saa 2:30 usiku kucheza dhidi ya KVZ.

Ratiba ya Mapinduzi Cup January 2, 2017

Azam vs Zimamoto saa 10:00 jioni

Yanga vs Jamhuri saa 2:15 usiku

Read More »

Mchezaji wa Simba afiwa na watato wake watatu


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI*
 Klabu ya Simba imepokea kwa mstuko mkubwa taarifa ya msiba wa watoto wa mchezaji wetu Juuuko Murshid vilivyotokea leo huko kwao nchini Uganda.

Vifo vya watoto hao watatu vimekuja katika kipindi hiki ambapo mchezaji wetu huyo wa kimataifa, akiwa kwenye maandalizi ya fainali za mashindano ya Afcon, yanayotarajia kuanza katikati ya mwezi ujao.

Tunajua uzito wa kufiwa na na watoto hao, na tunatambua uchungu aliona nao nyota wetu huyo, yeye pamoja na mkewe, lakini tunaamini Mungu atawapa subira na uvumilivu mkubwa ktk kipindi hiki kigumu wanachopitia.

Mwisho klabu inawatakia Wanasimba na Watanzania wote heri ya mwaka mpya 2017.

Imetolewa na. *Haji S Manara*

Mkuu wa Habari wa Simba Sc

Read More »

Bondia Francis Cheka atangaza ramsi kustaafu ngumi

Bondia maarufu nchini Tanzania Francis Cheka, jana ametangaza rasmi kustaafu mchezo wa msumbwi kwa kile alichokieleza ni ubabaishaji wa ma-promota pamoja na kutopata faida katika mchezo huo.
Cheka ambaye anakabiliwa na tuhuma za kuchukua pesa na kugoma kupanda ulingoni katika pambano lililokuwa limeandaliwa siku ya Krismasi, amesema amechoshwa na kile alichokiita kuwa ni utapeli wa mapromota, na kwamba sasa atajikita zaidi katika mapambano ya kuhamasisha vijana.
Akiwa amedumu kwenye ngumi nchini kwa takribani miaka 19, Cheka amesema mchezo huo umetawaliwa na majungu, na fitina huku watu wengi wakifikiri kuwa kuna pesa nyingi, wakati hakuna anachokipata zaidi ya umaarufu na kuhojiwa kwenye vyombo vya habari.

"Huu mchezo una majungu na fitina, hakuna faida yoyote zaidi ya kuhojiwa na waandishi wa habari, hakuna pesa, tunapata pesa gani, watu wanadhani tunapata pesa, nitabaki kucheza mapambano kwa ajili ya kuhamasisha vijana katika ngumi pamoja na kufanya biashara nyingine nipate pesa, nimedumu kwenye ngumi zaidi ya miaka 19, nimevumilia mengi" Alisema Cheka.

Read More »

SIMBA YAPAA KILELENI, YAISHUSHIA RUVU SHOOTING KIPIGO

Bao pekee la kiungo Ibrahim Mohamed ‘MO’ limeendelea kuifanya Simba ibakile kileleni kwa tofauti ya pointi nne (4) mbele ya wapinzani wao Yanga SC walioshinda jana December 28 kwa bao 4-0 dhidi ya Ndanda FC.Kwahiyo ushindi wa Simba unafanya tofauti ya Simba na Yanga kuwa ni ileile ya pointi nne baada ya timu zote kucheza idadi sawa ya mechi.Katika michezo nane iliyopita, Ruvu Shooting imeambulia sare moja huku ikiwa imepoteza mechi saba mbele ya ‘mnyama.’

Read More »

Azam FC yawatimua makocha wa Hispania



Azam FC imeamua kuwatimua makocha wake wa kigeni wakiongozwa na kocha mkuu Zeben Hernandez kutoka Hispania.

Uamuzi wa Azam umekuja baada ya mfululizo wa matokeo mabovu kwenye ligi kuu Tanzania bara msimu huu tangu ‘wahispaniola’ walipokabidhiwa mikoba ya kuinoa timu hiyo baada ya Stewart Hall kubwaga manyanga.

“Uongozi wa Azam FC umewatimua makocha wao leo mchana baada ya pande zote mbili kukubaliana kuvunja mkataba kutokana na matokeo mabaya kwenye ligi tangu walipowasili,” chanzo cha kuaminika toka ndani ya Azam FC kimeiambia shaffihdauda.co.tz.

Katika mechi 17 za VPL ambazo Hernandez alisimama kama kocha mkuu wa Azam FC, timu hiyo imeshinda mechi saba (7), imetoka sare mara sita (6) na kupoteza michezo minne (4).

Hadi sasa Azam ipo nafasi ya nne kwenye msimamo wa VPL ikiwa na pointi 27 baada ya kucheza mechi 17. Azam inazidiwa pointi 14 na Simba ambao ndio vinara wa ligi huku wakiwa nyuma kwa pointi 10 dhidi ya Yanga huku wakizidiwa pointi moja na Kagera Sugar.

Read More »

YANGA YAFANYA KWELI ,YAIPA NDANDA FC KIPIGO KIZITO

Ligi Kuu soka Tanzania bara imeendelea tena leo December 28 kwa Dar es Salaam Young Africans kucheza dhidi ya Ndanda FC, Yanga imefanikikiwa kuifunga Ndanda FC goli 4-0, magoli yakifungwa na Donald Ngoma dakika ya 4 na 21, Amissi Tambwe dakika ya 25 na Vincent Bossou.

Read More »

KRC Genk ya Mbwana Samatta yamtangaza kocha wa zamani wa Man United kuwa kocha mkuu


Ni siku moja imepita toka timu ya KRC Genk ya Ubelgiji inayochezewa na mtanzania Mbwana Samatta, itangaze kuachana na kocha wake mkuu Peter Maes kutokana na mfululizo wa matukio yasiyoridhisha katika michezo ya hivi karibuni.

KRC Genk baada ya kuachana na Peter Maes leo imemtangaza kocha mpya atayerithi nafasi ya Peter Maes, Genk imetangaza Albert Stuivenberg aliyewahi kuwa kocha msaidizi wa Man United chini ya Louis Van Gaal.

Kama humfahamu vizuri Albert Stuivenberg aliwahi kuifundisha timu za taifa za vijana za Uholanzi kuanzia mwaka 2006 hadi 2013 alikuwa akiifundisha timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17 na baadae 2013/2014 kuifundisha timu ya vijana ya chini ya umri wa miaka 21.

Read More »

Farid Musa kujiunga na klabu yake mpya ya Tenerife inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini Hispania


Baada ya kukwama kwa muda mrefu, hatimaye kijana Farid Musa anaondoka kwenda Spain kujiunga na klabu yake mpya ya Tenerife inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini Hispania (Segunda División) kwa ajili ya kucheza soka la kulipwa.

Afisa habari wa Azam FC Jafar Idd amethibisha safari ya Farid Musa kwa kuonesha tiketi iliyotumwa na timu ya Tenerife ambayo ndio ataitumikia kwa mkopo.

“Kama mtakumbuka tuliwaambia Farid Musa taratibu zake zinakwenda vizuri, aliitwa ubalozini akapeleka passport yake na mkataba wake na Azam FC. Ninapoongea na ninyi ni kwamba, klabu ya Tenerife ya Spain imetuma tiketi ya ya Farid Musa ambapo anatarajiwa kuondoka tarehe 28 (kesho) kuelekea Spain kujiunga na klabu yake,” anasema Jafar Idd wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Farid anataraji kuondoka kesho December 28 saa 5 usiku kwa ndege ya KLM kutoka Dar hadi Amsterdam ambapo ataunganisha hadi Barcelona kisha Tenerife.

Mjadala wa Farid ulikuwa mkubwa baada ya mchezaji huyo kuchelewa kuondoka kwenda kujiunga na timu yake mpya baada ya dili lake la kusajiliwa kwa mkopo kukamilika. Nyota huyo wa timu ya taifa amekuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu hadi nahodha wa timu ya taifa Mbwana Samatta aliwahi kuhoji.

Read More »

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lasema Mechi ya Simba na Yanga iko palepale

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema kuwa mechi ya ligi kuu Tanzania Bara ya mzunguko wa pili kati ya Simba na Yanga iliyokuwa imepangwa kuchezwa Februari 18 mwaka 2017 iko palepale kwa kuwa bado halijafikiria kuibadili tarehe hiyo.

Hatua hiyo inatokana na tarehe hiyo kugongana na kalenda ya CAF ya michuano ya Klabu Bingwa Barani Afrika iliyotolewa hivi karibuni na kuipanga Yanga kucheza mchezo wa marudiano kati yake na Ngaya de Mbe ya Comoro kati ya tarehe 17, 18 na 19 mwezi Februari 2017.

Afisa Habari wa TFF Alfred Lucas amesema kuwa hadi sasa shirikisho hilo kupitia Bodi ya Ligi halijafikiria kufanya mabadiliko yoyote kwenye ratiba hiyo, na kwamba ratiba itaendelea kubaki kama ilivyo hadi hapo itakapotangazwa vinginevyo.

"Ratiba imeshapangwa na haitabadilika, kila timu inajua itacheza lini, kuhusu ratiba ya CAF haiwezi kutuzuia kufanya mashindano yetu, kama kuna timu inacheza CAF inatakiwa ijipange, kila timu inatakiwa kuwa tayari wakati wowote ndiyo maana zinafanya matayarisho, zinaajiri makocha, zinasajili wachezaji , hiyo yote ni matayarisho kwahiyo sidhani kama watahitaji kupumzika na kutuharibia ratiba" Amesema Lucas

Jumatatu iliyopita Mtendaji Mkuu wa Bodi ya ligi Boniface Wambura akiwa kwenye kipindi cha 5Sports cha EATV, alisisitiza kuwa katika mzunguko wa pili wa ligi, ratiba haitakuwa tatizo, na kwamba haitabadilishwa badilishwa kwa kuwa katika upangaji wake kila kitu kilizingatiwa ikiwemo kalenda ya CAF.

Read More »

Matokeo ligi kuu ya Uingereza





Read More »

Kocha wa Mbwana Samatta afutwa kazi


Timu ya KRC Genk ya Ubelgiji leo kupitia tovuti rasmi ya timu hiyo imetangaza kusitisha mkataba na aliyekuwa kocha wake mkuu Peter Maes kutokana na kutoridhishwa na matokeo ya timu hiyo kwa mechi za hivi karibuni.

Peter Maes anafutwa kazi ikiwa imebakia siku moja kabla ya KRC Genk kucheza mchezo wake wa Ligi Kuu Ubelgiji dhidi ya KAA Gent utakaochezwa kesho December 27 katika uwanja wa nyumbani wa Genk Luminus Arena.

Read More »