Klabu ya soka ya Yanga imeiomba Wizara ya Michezo ya Zanzibar iwaruhusu kuutumia Uwanja wa Amaan.




Yanga wamechukua hatua hii kufuatia Serikali kuzizuia klabu za Yanga na Simba kuutumia Uwanja wa Taifa kutokana na uharibifu wa miundombinu uliofanywa na mashabiki.


Mchambuzi
Nina imani kubwa kuwa TFF kwa ushirikiano na ZFF watalikataa ama kulipinga hili kwa sababu kimsingi uwanja wa Amani upo Zanzibar ambapo ligi yao inafanya kazi kwa kujitegemea na pia kwenye haki za fedha za Udhamini hii haikuwa imependekezwa kwa maana ya baadhi ya vilabu kutokuwa pia na bajeti ya kufika huko katika mwaka wa mahesabu wa kifedha wa kila klabu ambao hufungwa mapema baada ya maandalizi ya mahesabu ya mahesabu ya mwaka mzima wa matumizi ya klabu husika. Kwa hili hata vilabu vina haki ya kupinga hadharani.
Sheria za ligi yoyote huitaji nadhani vilabu kuchezea michezo ya ligi katika zonal area inayotambulika na chama kinachoendesha ligi hiyo isipokuwa kwa issues za kuweka neutrality grounds, kuepuka fujo kwa maana ya kutokuwepo kwa football hooligans na vitu kama hivyo. Sidhani kama hii ni sababu ya Yanga kwa sababu hakuna maafa, hawajaomba kwa mchezo mmoja wa kuweka usawa "netrality" ili kuamua matokeo tatanishi ama yaliyolingana na sidhani kama TFF italipitisha hili.

Vilabu vya Wales wengi wanaweza kuchukulia mfano kama Cardiff na Swansea lakini hawajui kuwa timu hizi zinatambulika kuwepo kwenye mfumo ule wa championship na Premier league na zinapanda daraja kama nyingine. Sheria ya Uingereza kwa vilabu vyake na vile vya visiwa vyake ni kuwa, zile zilizokuwa wanachama rasmi wa FA na zinazofanya kazi chini ya kanuni za ligi za PL pekee ndo zenye mamlaka ya kuhusika na ligi Ile kwa namna yoyote na vilabu hivi vya Wales vimeandikishwa chini ya mwamvuli wa FA.

Hii issue chama cha soka cha Zanzibar, ZFF pia kinaweza kuathirika kwa maana ya matokeo ya idadi ya mashabiki wa ligi ya Nyumbani kwa maana ligi ya Zanzibar.

Hii iliwahi kutokea mwaka 1998 kule Uingereza. Wimbledon alikuwa ni mwanachama halisi wa FA. Na kwa sababu FA ilimruhusu kuchagua uwanja wa kuchezea yeye akaamua kwenda jamhuri ya Ireland kufanya uwanja wa nyumbani. Kule chama cha soka kikastuka kikagundua namna ambayo watu watahitaji kuona zaidi ligi kuu ya Uingereza kuliko ligi ya Irish. Kikapinga suala hili na kwa sababu lilikuwa ni haki yao na masilahi yao, klabu ya Wimbledon akazuiwa ombi lake.