Mourinho amdhihaki tena Arsene Wenger



Jose Mourinho amesema Wenger anapewa heshima asizostahili, kwani taji la mwisho ametwaa miaka 14 iliyopita

Jose Mourinho amemdhihaki Arsene Wenger kwa mara nyingine tena baada ya kudai kuwa meneja huyo wa Arsenal ameshindwa kuunda timu ya kutwaa ubingwa kwa muda wa miaka 14.

Bosi huyo wa Gunners kwa mara ya mwisho alitwaa ubingwa wa Ligi Kuu Uingereza mwaka 2004, ingawa ameiongoza timu yake kutwaa Kombe la FA mara tatu tangu hapo.

Kabla ya sare ya Manchester United ya 1-1 dhidi ya Arsenal Jumamosi, Mourinho alimponda Wenger akidai kuwa meneja huyo wa Arsenal anapata heshima asizostahili kuliko yeye.

Mourinho alimbatiza Wenger jina la “Mtaalamu wa kushindwa” yaani “Specialist in failure” mwaka 2014, na bosi huyo wa Manchester United alizidi kumwandama Mfaransa huyo kabla ya mechi ya Jumamosi dhidi ya Arsenal.

“Taji langu la mwisho Ligi Kuu Uingereza lilikuwa miezi 18 iliyopita, si miaka 18 iliyopita,” alisema akirejea mwaka wa mwisho Arsenal kutwaa ubingwa 2004. “Ilikuwa miezi 18 iliyopita lakini sidhani kama Napata heshima yangu.”

MOURINHO ALIMPONDA WENGER BAADA YA SARE YA 1-1.

Kukosa mafanikio kwa Wenger katika muongo mmoja uliopita – tangu walipotinga fainali ya Ligi ya Mabingwa 2006, Gunners wameshinda mataji mawili ya Kombe la FA jambo linalomfanya Mournho kumshambulia Wenger kwa maneno.

Katika mahojiano na ESPN Brasil baada ya sare ya 1-1 Jumamosi, meneja huyo wa zamani wa Chelsea hakuweza kujizuia kumponda Wenger tena.

“Nilisema jana kwenye mkutano wa waandishi,” Alisema Mourinho Jumamosi. “Meneja wa Arsenal hajatwaa ubingwa kwa muda wa miaka 14. Sijashinda kwa muda wa miezi 18 tu.”

Licha ya timu ya Wenger kuwa pointi sita mbele ya United, ni dhahiri kuwa ipo njia moja ya kumziba mdomo Mourinho.

Arsenal mara zote wanaweza kutinga nne bora kama kawaida, lakini bila ya ubingwa wa Ligi hawana cha kushangilia.

Jamie Carragher amesema Arsene Wenger amekuwa kocha mahiri, na kikosi cha Arsenal kimekuwa kikifanya vizuri wachezaji wake wanapokuwa katika ubora wao, lakini amesisitza kuwa msimu huu hawana kisingizio tena kwa sababu kila kitu kimo mikononi mwao.