Tunda asema "Nimefanya Video Karibia 10 Lakini ya Diamond Mnaniuliza Kila Saa, Who is Diamond Motherf**** – Tunda
Tunda amechoka kuulizwa maswali kuhusiana na kuonekana kwenye video ya Diamond ya wimbo Salome aliomshirikisha Ray Vanny.
Ni kwasababu anajiuliza, iweje ameshaonekana kwenye video takriban 10, lakini tangu aonekane kwenye video ya Diamond, swali limekuwa lile lile na ni kama vile watu ndio wameanza kumuonea kupitia video hiyo.
Kutokana na kuchoshwa na swali hilo, Tunda anayedaiwa kurudiana na mpenzi wake Young Dee, amempa jibu kavu mtangazaji wa Jembe FM, Natty E aliyemrushia swali lile lile limkeralo.
“Nimefanya video ngapi? Nimefanya video karibia 10 lakini hii ya Diamond mnanifanyia interview kila saa,” Tunda alimjibu Natty.
“Diamond, Diamond, who is Diamond motherf*cker. Weka hiyo kwenye gazeti lako,” aliongeza.
Natty alijikaza na kumjibu ‘Anyway, Unaweza acha hilo swali la kuhusu Diamond, it’s not a big deal.’
Tunda alijibu kikauzu zaidi, “Maswali yote jibu lake ndio hilo.”
Anachoshindwa kukielewa Tunda ni kuwa kushiriki kwenye Salome ya Diamond ni hatua kubwa zaidi katika career yake so far hivyo swali hilo hawezi kulikwepa! Hadi sasa video hiyo ina views milioni 9.2 na ni video ya Diamond inayopata views nyingi kwa kasi kuliko zote alizowahi kutoa.
Fredrick Bundala