Jinsi ya kufungua blog yenye kuleta wasomaji wengi na kukufanya utajirike na blog yako
Hatua ya kwanza kabisa ya kutengeneza website (haijalishi kama wewe ni webprogramer au hujui chochote kuhusu programing) au mambo muhimu ya kuzungatia kabla ya kuamua kufungua au kutengeneza website .
1. Weka mipango Kabla(make a plan).
Kila kitu hapa ulimwenguni kikifanyika bila ya kuwa na mpangilio huwa ni kibaya au huwa hakivutii kama mtu aliyekaa chini na kupangilia kazi yake. Kwa hiyo kabla hujaanza kutengeneza website unatakiwa kupanga vizuri kuhusu website yako, unatakiwa kujua itakuwa inahusu nini, kama ni kuhusu company yako, au ni ya kufurahisha jamii. Umuhimu wa kupanga ni kwamba utaweza kujua vizuri hasa wakati unafanya hosting(kuhifadhiwa mafaili yako) kujua kuwa ni nani anatoa hosting services nzuri kwa ajili ya website yako au nani ana server(computer maalumu ya kutunza mafaili yako ya website) nzuri kwa ajili ya webiste yako pia kuweka plan kutakusaidia kuchagua a programmer (injinia wa kutengeneza website) kama ukiwa hujui kabisa kuhusu kutengeneza website Pia itakusaidia kujua Gharama za pesa au matumizi ya website yako. Kwenye blog hii nitatoa maelekezo ya kumsaidia mtu anayejua basic skills za website sio lazima ukawa professional ndio uweze kutengeneza professional website ukinifuatilia kwa makini maelekezo kwenye blog hii utaweza kutengeneza website kama professional. Ninasistiza kuwa kama utataka kujua viziri jinsi ya kutengeneza kupitia blog hii lazima ujifunze au uwe na ufahamu wa msingi(basic knowledge) wa HTML, au CSS ili uweze kutengeneza website yako.
2. Ubunifu(Creativity)
Kuhusu ubunifu ni kwamba watu huwa hawafikilii kuhusu kuwa wabunifu katika kazi ya kutengeneza website, Utakuna mtu anakurupuka tu na kuweka kila kitu anachojua kwenye website na kupanga anavyotaka kisha akaita hii ni website au hii ni blog ni sawa ila ukifika wakati wa kufanya mashindano ya biashara au kuweza kupata trafic(watu wanaotembelea website yako kwa mwezi) ya kutosha hapo itategemea wewe umeweza vipi kufanya ubuifu au website yako imetengenezwage, pia kama unategemea kupata wadhamini wa kuweka matangazo kwenye website yako basi itategemea ni jinsi gani wewe umeweza kubuni website yako na kuitengeneza vizuri ili kila anayekuja kupitia website yako aweze kuduri tena na kuangalia nini kilichomo ndani ya website yako.
Watu wanaweza kusema kuwa Ubunifu(creativity) huwezi kusomea maana ni kipaji cha mtu , ni kweli kabisa na ila ni kwamba unaweza kukiendeleza kipaji chako kama utaweza kuwasoma(hahaha kiswahili cha kisasa) nina maana kama utaweza kujifunza kutoka kwa baadhi ya website ambazo ni nzuri na pia hata bloggers wazuri (maarufu) kamaMichuzi Tanzania.
Pia Ubunifu huu unachangia hata jinsi unavyoandika makala za website yako na ni jinsi gani ulichokiandika kinavyovutia watu, haka kama unategemea kupata pesa kupitia website yako basi unatakiwa kuangalia kwa umakini mkubwa jinsi unavyoandika kwenye website yako na jinsi ulivyopangilia maandishi yako, kama hujui kuandika vyema ni vizuri ukapitia kwenye mtandao kwani kuna watu wengi wanaelekeza jinsi ya kuandika kwa kuvutia.

3.UVUMILIVU
Ninapenda kuwa muwazi katika swala hili la kutengeneza website , kikubwa unachotakiwa kuwanacho ni Uvumilivu(hahaha…ni kama wakristo wamekuwa kwa muda mwingi wakingojea masihi ambaye ni kristo yesu na sasa ni miaka zaidi ya 2000 bado hajaja…wow ni uvumilivu wa hali ya juu, hahaha… ni ninaamua kukufanya walau utabasamu maana naona umekuwa makini sana) zao. Kweli ni kwamba watu wengi siku hizi wanatengeneza hela nzuri sana kupitia website zao. Sasa kwa hili swala uvumilivu ni kitu cha msingi sana na cha muhimu sana. Ninazungumzia uvumilivu ni kwa wale wanaotaka kupata pesa kupitia website.
Zifuatazo ni baadhi ya ‘ideas’ ambazo zinaweza kutengeneza blogs zenye kuleta wasomaji wengi na pia zikaleta mchango chanya katika jamii.

NOTE:UPO HURU KUTUMIA ‘IDEAS’ HIZI KUTENGENEZA BLOGU YAKO
1.Fursa kwa wajasiriamali :
1.Fursa kwa wajasiriamali :
Waweza anzisha blogu mahsusi kwa fursa motomoto kwa wajasiriamali wa sasa na wale wanaotaka kuwa wajasiriamali. Blogu hii haitojihusisha na makala kuhusu ujasiriamali (maana wapo wengi wanaandika kuhusu hilo) badala yake itajikita katika kuweka taarifa motomoto za upatikanaji wa mafunzo ya ujasiriamali, mikutano, semina, mikopo, na asasi mbalimbali zinazosaidia wajasiriamali. Waweza pia weka links za blogs zinazohusiana na ujasiriamali ili kufanya blogu hii iwe nyumbani kwa wajasiriamali.
2. Shule za Kata:
2. Shule za Kata:
Habari nyingi zinaandikwa kuhusu shule za kata. Ili kuleta upekee blogu yako hii itajikita kueleza mafanikio , changamoto na jinsi shule za kata zinavyojitahidi kujikwamua. Takwimu na picha ni muhimu sana kwa blogu hii. Pia unaweza onyesha program mbalimbali za maendeleo zinazosaidia shule za kata. Kuhoji wanafunzi wa shule husika, na kuonyesha maisha ya shule za kata. Lengo ni kusaidia wazazi na walezi kutambua mazingira na maendeleo ya shule wanazopeleka watoto wao, au wanazotarajia kupeleka watoto wao. Maana wapo wengi mtoto toka Form 1 hadi Form 4, hawajakanyaga shule anaposoma mtoto.
3.Picha Uwanjani:
3.Picha Uwanjani:
Kuna blogu nyingi zenye habari na michezo na burudani. Ili kuleta upekee, blogu yako hii itakuwa ni ya picha tuu. Tena picha kali zaidi , ikisindikizwa na Facebook page, yenye kusheheni picha za matukio mbalimbali ya burudani na michezo. Si unajua kuwa picha inatoa maneno maelezo zaidi ya Maneno ? Ndio hivyo, hakikisha picha unazoweka zinabeba ujumbe au taarifa fulani, ambayo hautoelezea kwa maneno ila mtazamaji atajionea mwenyewe. Kumbuka kutaja vyanzo vya picha ambazo haukupiga wewe mwenyewe.
4.Nukuu zetu:
4.Nukuu zetu:
Unakumbuka nukuu kama vile “…ukitaka kula ukubali kuliwa”?. Basi waweza tengeneza blogu maalum ya nukuu toka Tanzania. Waweza zigawa katika makundi ya Siasa, Jamii, Teknolojia, Uchumi, Michezo, Elimu, n.k. Usisahau ile nukuu ya Tanzania ni muungano wa visiwa vya Zimbabwe, Pemba na Tanganyika. Kumbuka kupata nukuu sahihi, na ikiwezekana utaje kabisa nani alitoa maneno hayo. Blogu hiyo ya nukuu zetu, itaburudisha na kuelimisha pia, na kutukumbusha wapi tunatoka, na wapi wapi tutarajie kuenda.
5.Skonga:
5.Skonga:
Blogu hii itakuwa maalum kwa wanafunzi na wazazi. Ni kama vile shule, ila shule ya mtandaoni, ambapo Matokeo mbalimbali ya Form 4, 2, QT, FORM4, yatawekwa. Msaada kwa wanafunzi kwa njia ya ‘materials’ ya kujisomea yataweka, na makala zenye kujaa mbinu za kusoma, changamoto za maisha ya kishule, habari motomoto zihusuzo elimu zitawekwa humu. Mambo mengine ya maisha ya kishule kama vile majina ya walimu, ambayo wanafunzi huwatunga yatawekwa humu.
6.Wakali wa Bongo:
6.Wakali wa Bongo:
Badala ya kuandika habari za watu maarufu na mashuhuri kama udaku, blogu hii ya wakali wa Bongo, itajitofautisha kwa kuangalia maisha ya watu hawa katika muonekano chanya. Blogu itachambua changamoto wanazokumbana nazo, nini wamejifunza kuhusu mafanikio, na wanafanya nini kuendelea kubaki kuwa na mafanikio. Pia blogu itaangalia wakali wengine waliopo katika jamii lakini hawajapata kuwa mashuhuri kama vile wanafunzi waliofaulu kwa viwango vya juu kabisa katika masomo yao. Itaangalia pia biashara zinazotamba Tanzania, Shule zinazotamba na zilizowahi kutamba kama vile TAMBAZA, wanasiasa, na asasi zisizo za kiraia. Blogu hii itanogeshwa na mahojiano na wahusika, picha, na historia mbalimbali. Unataka kuanza blogu hii ? Embu fuatilia na kuandika ukali wa shule ya TAMBAZA. Enzi hizo TAMBAZA ilivyosifika kwa fujo lakini pia kwa ubora wa wanafunzi.
7.Mkali wa Facebook:
7.Mkali wa Facebook:
Blogu hii ni mahsusi kwa mambo yanayovutia kuhusiana na Facebook. Mambo kama vile picha zilizopata ‘likes’ nyingi (zisiwe picha za mtu binafsi), status kali, au comments zenye mvuto zaweza kuwekwa humo. Mambo mengine ni taarifa za kiufundi kuhusu applications mbalimbali zinazopatikana Facebook kama vile BranchOut, na mambo mapya ya matumizi ya Facebook yanayoletwa na kampuni ya Facebook kama vile Timeline.