SIMBA YAPAA KILELENI, YAISHUSHIA RUVU SHOOTING KIPIGO
Bao pekee la kiungo Ibrahim Mohamed ‘MO’ limeendelea kuifanya Simba ibakile kileleni kwa tofauti ya pointi nne (4) mbele ya wapinzani wao Yanga SC walioshinda jana December 28 kwa bao 4-0 dhidi ya Ndanda FC.Kwahiyo ushindi wa Simba unafanya tofauti ya Simba na Yanga kuwa ni ileile ya pointi nne baada ya timu zote kucheza idadi sawa ya mechi.Katika michezo nane iliyopita, Ruvu Shooting imeambulia sare moja huku ikiwa imepoteza mechi saba mbele ya ‘mnyama.’