Lipuli FC yapanda daraja ,sasa kucheza Ligi Kuu


Timu ya Lipuli ya mkoani Iringa imerejea ligi kuu Tanzania bara baada ya kupita miaka 17 tangu iliposhuka dara na mkoa huo kukosa timu ya Ligi ya Vodacom kwa kipindi chote hicho.

Kocha msaidizi wa zamani wa Simba raia wa Uganda Richard Amatre ndiye ameipandisha timu hiyo baada ya kusota nayo kwa miaka mitatu ikiishia katika nafasi za pili na tatu.

Amatre alisema "haikuwa kazi rahisi, lakini jitihada zake na wachezaji wake ndivyo vimewasaidia kupanda na kufuzu ligi hiyo ambayo ndiyo ya kwanza kwa ukubwa Tanzania Bara"

“Nawapongeza sana viongozi wa timu wachezaji na wananchi wote wa mkoa wa Iringa, kwa umoja na ushirikiano wao waliouonyesha hadi kufanikiwa kuipandisha timu ligi kuu, lakini pamoja na kupanda bado tunakazi kubwa lengo ni kuhakikisha tunadumu na kupata mafanikio kwenye ligi ya Vodacom,”amesema Amatre.

Kocha huyo amesema walistaili kupanda msimu kutokana na mapambano waliyopitia hadi kufikia hapo lakini pia ubora wa kikosi chake ambacho kilikuwa na nyota wengi wenye ubnora wa hali ya juu kuzidi timu zote zilizokuwa kwenye kundi lao.

Mganda huyo amesema mia yao ilikuwa nikurejea ligi kuu nakufanya mapindunzi ya soka katika mkoa wao wa Iringa, hivyo wanajipanga ili wasishuke daraja tena.

“Mashabiki wetu waendelee kutusapoti na kamwe hatuwezi kuwaangusha tutajituma kadri ya uwezo wetu ili kuwapa matokeo mazuri kama tulivyokuwa tunafanya huku katika ligi daraja la Kwanza”, alisema Amtri.

Lipuli inaongoza kundi hilo ikiwa na alama 29 huku ikibakiwa na michezo miwili mikononi mwao.