Showing posts with label Habari. Show all posts

RC Makonda atema cheche " Nisemeni, Mkichoka Mtanyamaza"


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kelele zinazoendelea dhidi yake ni dalili za mafanikio katika vita dhidi ya dawa za kulevya.
Makonda ameyasema hayo jana alipokuwa mgeni rasmi katika tamasha la Twendezetu Kigamboni lililofanyika katika wilaya.

Amesema, mapambano dhidi ya dawa za kulevya ni ya kufa au kupona.

“Mfahamu kuwa tunapambana kati ya mauti na uzima, kelele, mwangwi vinavyoendelea sasa ni dalili njema kwamba tunaendelea kunyooka,”amesema Makonda.

Makonda alisema Dar es Salaam ya sasa anaifananisha na chuma kilichopinda na sasa kiko katika hatua ya kunyooka hivyo lazima zitokee kelele nyingi kama ambavyo zinaendelea sasa.

“Huwezi kufanya kazi ya kunyoosha chuma bila kusikia mwangi, kelele na maumivu kwa sababu kazi ya kukomboa vijana dhidi ya dawa za kulevya si rahisi,” amesema Makonda.

Amesema katika kipindi hicho ambacho amekiita kuwa ni cha kulinyoosha Jiji la Dar es Salaam ni lazima kelele zisikike, uonekane moto unaoacha maumivu makali na baada ya hapo ije picha ya chuma kilichonyooka ambayo ndio picha ya Jiji la Dar es Salaam itakayokuwa imenyooka.

Amesema kelele hizo zitapita na mwisho lazima kufika ng’ambo ya pili pasipo na dawa za kulevya, kwenye taifa lililojengwa na uchumi imara.

Amelipongeza Jeshi la Polisi kwa jitihada zake za kuhakikisha dawa za kulevya zinatokomezwa ambapo alisema hivi sasa katika Jiji la Dar es Salaam dawa hizo zimepungua.


“Nitoe pongezi kwa Jeshi la Polisi dawa za kulevya zimepungua sasa Dar es Salaam na pia niwapongeze pia vijana ambao wanaendelea kutoa taarifa,” alisema Makonda.

Aliwaasa wananchi kushirikiana na Rais John Magufuli ambaye anafanya jitihada kuijenga Tanzania ya kesho iliyo bora. Kuhusu Kigamboni alisema anatarajia kuiona Kigamboni ikiwa mji wa mfano ambao haujaharibiwa na matendo yasiyofaa ikiwa ni pamoja na uhalifu na vijana walioharibika kutokana na matumizi ya dawa za kulevya badala yake kuwe na vijana wachapakazi.

“Watu watakapokuja Kigamboni wakute ni mji msafi, salama, uliopangika unaofaa kupumzika… mji ulio salama usio na uhalifu,”amesema Makonda.


Amewataka wakazi wa wilaya hiyo kushirikiana na Mkuu wa Wilaya hiyo, Hashim Mgandilwa na viongozi wake katika kutimiza ndoto hiyo ya kuifanya Kigamboni tulivu na salama.

Amewaasa wazazi kuhakikisha wanafuatilia mienendo ya watoto wao kuhakikisha hawajiingizi katika matumizi ya dawa za kulevya na pia vijana kuchungana wao wenyewe.

Mkuu wa Wilaya hiyo, Mgandilwa alisema lengo la tamasha hilo ni kuzitambulisha fursa zilizopo katika wilaya hiyo, kuwakutanisha vijana kupiga vita dawa za kulevya na pia kuiunga mkono serikali katika kufanya mazoezi.

Tamasha hilolilihudhuriwa pia na Mbunge wa Jimbo hilo, Dk Faustine Ndungulile Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Rahel Mhando na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo.

Read More »

Breaking News:Mbunge wa Arusha Godbless Lema apata dhamana

Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Mjini baada ya kupitia hoja za mawakili pande zote imemwachia kwa dhamana Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless Jonathan Lema. Ameachiwa kwa dhamana ya masharti ya wadhamini wawili na kusaini bondi ya shilingi milioni moja.

Read More »

KIMENUKA TENA!!!! Sauti: Askofu Gwajima aelezea sakata zima la Makonda kutumia vyeti vya mtu mwingine




Siku kadhaa baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kusema kuwa hawezi kujibu madai ya mitandao ya kijamii kuwa alitumia vyeti vya mtu cha kidato cha nne, Askofu Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima ameibuka na kusema kuwa ni kweli alitumia vyeti hivyo.

Askofu Gwajima amesema kuwa anamfahamu sana Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na kuwa jina lake halisi ni Daudi Bashite na kwamba hilo la Paul Makonda ni la mwenye vyeti hivyo.
Aidha, Askofu Gwajima amedai kuwa anavyovyeti vya Daudi Bashite vinavyoonyesha kuwa hakufaulu na kwamba atashangaa kama Waziri wa Elimu, Prof. Ndalichako atalifumbia macho jambo hili. 
Pia ametishia kuwa, kama mamlaka husika hazitachukua hatua haraka basi yeye atatoka hadharani na vyeti hivyo.

Hapa chini ni sauti ya Askofu Gwajima akihubiri kanisani kwake.

Read More »

Wema Sepetu atangaza kuhamia CHADEMA Angalia video hapa

Msanii wa filamu nchi Tanzania Wema Sepetu ametangaza rasmi kukihama Chama cha Mapinduzi CCM na kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)


Akizungumza na waandishi wa habari leo akiwa ameambata na mama yake mzazi nyumbani kwao Sinza Jijini Dar es Salaam, Wema amesema sababu kubwa ya kuhamia CHADEMA ni ili kupata nafasi ya kupigania demokrasia anayodai kuwa inapotea nchini Tanzania.

Sababu nyingine aliyoieleza Wema ni kutelekezwa na CCM licha ya kujitolea kutoa mchango wake kwa chama hicho wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kiasi cha kuwa hatarini kumwagiwa tindikali visiwani Zanzibar.

"Kuanzia sasa mimi siyo tena mwanachama wa CCM, na muda mfupi ujao nitachukua kadi yangu ya CHADEMA... Nimeamua kuingia CHADEMA kwa sababu nataka kupigania demokrasia, laiti ningejua, ningeingia zamani sana, najua nimewahi kusema kuwa nitakufa nikiwa CCM, lakini sikujua kama itakuwa hivi, laiti ningejua mapema basi nisingesema vile na ningejiunga CHADEMA muda mrefu sana".Amesema Wema Sepetu

Amesisitiza kuwa hajaamia CHADEMA kwa sababu ya pesa kama ambavo imekuwa ikidaiwa, bali ni kwa ajili ya kupigania demokrasia, na kuweka wazi kuwa kuanzia sasa ameingia kwenye mapambano ya kupigania demokrasia akiwa kwenye chama ambacho anaamini kuwa ni chama peke chenye uwezo wa kurejesha demokrasia inayopotea.

"Sijachukua pesa yoyote kutoka CHADEMA, kama nimechukua hata shilingi 10,000 ya CHADEMA basi kaburi la baba yangu huko Zanzibar litikisike" - Amesema Wema

Wema pia amejibu kuhusu baadhi ya wasanii kuidai CCm ambapo amesema "Ni kweli kuna madeni mengi wasanii tunaidai CCM, lakini kila wakati tukidai tunaambiwa tukamdai JK" - Wema Sepetu

Baada ya Wema kukabidhi kadi ya CCM, mama yake pia amerudisha kadi ya CCM na kusema "Tutatembea Tanzania nzima kuinadi CHADEMA". Kauli hiyo ilikuja baada ya mama huyo kueleza jinsi ambavyo CCM haikumtendea haki

Kuhusu sauti zilizosambazwa mitandani zikionesha Mama Wema akiongea na Steve Nyerere, mama Wema amesema "Kuhusu sauti zinazosemwa kuwa ni mimi na Steve Nyerere, siwezi kulizungumzia hilo maana sijazisikia"

Read More »

MZEE WA UPAKO: Atoa Onyo Kali kwa Nay wa Mitego Baada ya Kudai Anakuja na Kanisa lake


Baada ya hivi karibuni msanii wa hip hop, Nay wa Mitego kutangaza kuwa atafungua kanisa lake ambalo litakuwa si la biashara bali ni la kumuabudu Mungu aliye hai, Mchungaji maarufu nchini, , Lusekelo Anthony aka Mzee wa Upako amemuonya kutomchezea Mungu.

Mzee wa upako ameyasema hayo alipotafutwa na E-News ya EATV baada ya kuulizwa maswali juu ya kauli hiyo.

“Kama unakuja kanisani kwa maana kuna biashara, nakupa miaka hii mitatu sio utatembelea ndala utatembelea kucha, ni mtoto mdogo sana hana akili. Mungu hataniwi, anafanya kufuru, kama ana mama yake amemzaa amuonye. Mimi biblia nimesoma na hizo lugha zake nyepesi zitamtokea puani, asithubutu kufanya kanisa kama biashara. Baada ya miaka hii mitatu atajua kwamba kuongoza watu sio kama kuongoza ngo’mbe hakuna jambo gumu kama kuongoza watu wenye akili kama wewe wenye ufahamu kama wewe, wapo watu wengi walianzisha makanisa kwanini walifunga, ujinga hujui ni ujinga ni utoto,” Alisema Mzee wa Upako.

Read More »

Diamond naye ajikuta mikononi mwa polisi

Mwanamuziki Diamond Platnumz jana ameripoti Kituo Kikuu cha Polisi cha Usalama Barabarani baada ya video yake kusambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonyesha akiendesha gari bila kufunga mkanda huku akiachia usukani na kucheza ndani ya gari.

Daimond ambaye alikuwa ndani ya gari hilo pamoja na mpenzi wake, Zarinah Hassan, mama yake mzazi na mtoto wake walikuwa wakicheza wimbo mpya wa Diamond, Marry You aliomshirikika Ne-Yo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diamond ameweka picha akiwa na Kiongozi wa Kikosi cha Usalama Barabara, Kamanda Mpinga ambapo amewataka vijana wenzake kuhakikisha wanachukua tahadhari pindi wanapoendesha magari na kutumia barabara. Lakini pia ameeleza kuwa amelipa faini kwa mujibu wa sheria kutokana na kukiuka sheria za usalama barabarani.


“Leo nilireport kituo kikuu cha polisi wa usalama barabarani kutokana na Vidoe Clip tuliyopost naendesha gari barabarani bila kufunga mkanda na pia kuachia usukani na kucheza…. Nikapewa Onyo na Kulipa faini kulingana ya Mujibu wa sheria… tafadhali watanzania na Vijana wenzangu… tuhakikishe tunafunga mikanda pindi tupandapo na tuendeshapo Magari Maana ni Hatari kwa Maisha yetu na inaweza kukupeleka kunyea debe pia…🙏” ameandika Diamond

Read More »

Manji athibitika kutumia Madawa ya Kulevya, kupandishwa kizimbani leo

Hatimaye imedhibitika kuwa Mwenyekiti wa Timu ya soka ya Yanga na Mfanyabiashara mkubwa nchini Tanzania Yusuph Manji anatumia madawa ya kulevya na leo atapandishwa kizimbani kwa tuhuma hizo akiwa pamoja na watuhumiwa wengine wanaoshikiliwa kwa sakata kama hilo.

Katika Kipindi cha michezo katika redio moja nchini Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna, Simon Sirro amethibitisha kuwa vipimo vya Mkemia Mkuu wa Serikali alivyofanyiwa Manji vinaonyesha kuwa ni Mtumiaji wa Madawa ya kulevya (Hakuyataja aina yake) na kusisitiza kuwa leo mtuhumiwa huyo atapandishiwa kizimbani kujibu shitaka hilo.

Akielezea afya yake tangu alazwe Hospitali, Kamanda Sirro amesema kuwa mwenyekiti huyo wa yanga yuko vizuri na sasa ameruhusiwa kutoka Hospitalini na kurejeshwa mahabusu polisi kusubiri kupandishwa kizimbani.

Sirro amesema kuwa habari kamili kuhusu sakata hilo na watuhumiwa wengine wakiwemo wasanii waliokamatwa zitatolewa leo mbele ya wanahabari Jijini Dar es Salaam.

Read More »

Makonda aagiza mume wa muigizaji Shamsa Ford ( Chidi Mapenzi ) akamatwe

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ameagiza kukamatwa kwa mfanyabiashara maarufu nchini Chidi Mapenzi ambaye ni mume wa msanii maarufu wa filamu nchini Shamsa Ford kwa ajili ya mahojiano kuhusu dawa za kulevya.


Makonda ametaja jina la Chidi Mapenzi leo wakati akihitimisha mkutano wa uzinduzi wa awamu ya tatu ya vita dhidi ya dawa za kulevya katika mkoa wa Dar es Salaam, ambayo imeambatana na kukabidhi orodha mpya ya majina ya watuhumiwa wengine 97 kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Dkt. Rogers William Sianga.
Mara baada ya kupokea majina hayo, Kamishna Sianga amesema kuwa atayashughulikia na atahakikisha kila mtu anakamatwa na kushughulikiwa bila kumuonea mtu kwa mujibu wa sheria iliyounda mamlaka hiyo.


Jina lingine lililotajwa leo ni Mfaume Kiboko, ambapo Kamishna Sianga ameagiza pia akamatwe na apelekwe kwake haraka iwezekanavyo.

Katika hotuba yake, Mh. Makonda pamoja na kuweka wazi kuwa moto wa vita hiyo ndiyo unaanza kuwaka sasa, amewaonya watu wote ambao wanakaidi amri yake ya kuripoti polisi na kuwatangazia vita zaidi,huku akisema yeye kama mkuu wa mkoa ana mamlaka yote ya kumuita mtu yeyote na ikiwezekana kumfukuza kwenye mkoa wake.

"Ukiitwa polisi nenda, hizi mbwembwe nyingine achana nazo, hizo mbwembwe siyo kwenye utawala huu wa Magufuli, na siyo kwenye utawala na Makonda, Mwingine anasimama kabisa na kifua chake eti hawezi kwenda kwa sababu eti Makonda ni kijana mdogo, sasa kama Makonda ni mdogo hawezi kukuita wewe, atapajua shimoni ni wapi, Pia nina mamlaka ya kukufukuza kwenye mkoa wangu endapo nitajiridhisha kuwa wewe ni hatari kwenye mkoa wangu" Amesema Makonda 

Makonda amesema atatumia sheria mpya ya mwaka 2015 kuwashughulikia wote wanaohusika bila kujali ni nani, na kufafanua kuwa sheria hiyo inaelekeza pia adhabu kwa watumiaji na kuwataka watu wanaokosoa uamuzi wake wa kutaja majina waungane naye, kwa kuwa wao ndiyo waliotaka majina hayo awali

"Sheria mpya ya mwaka 2015 inasema mtumiaji wa dawa za kulevya atafungwa jela miaka mitatu, kuna wengine hakuna sheria ya kumuadhibu mtumiaji, hawahui sheria........Kuna wengine wakati ule wa Kikwete, aliposema ana majina walitaka ayataje, sasa leo Makonda anataja wanaanza kelele, nale ninayo majina mengine 97, na haya ndiyo yana watu wazito zaidi, na yataleta mtikisiko zaidi"

Pia ametaja baadhi ya mbinu mpya ambazo hutumiwa na wasambazaji wa dawa za kulevya kuwa ni pamoja na kutumia mitungi ya gesi, pamoja na kuwatumia wauza vitumbua mitaani.

Kwa upande wake Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Simon Sirro, amesema tangu Februari 01 hadi 12 mwaka huu, jumla ya watuhumiwa 311 wamekamatwa na kuhojiwa wakiwemo 77 waliotajwa na Makonda.

Amesema kati ya hao 311, watuhumiwa 117 walikutwa na vielelezo.

Read More »

Waziri Mkuu Akabidhiwa Kazi Ya Kupambana Na Dawa Za Kulevya

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemkabidhi Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa kazi ya kuzuia na kupambana na dawa za kulevya akiwa kama Mwenyekiti wa Tume ya Kudhibiti Dawa hizo nchini.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam wakati akiwaapisha Kamishna Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji, Anna Peter Makakala, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers William Sianga pamoja na mabalozi watatu Mhe. Omary Yusuph Mzee, Mhe.Joseph Edward Sokoine pamoja na Mhe. Grace Aron Mgovano aliowateua hivi karibuni.

Dkt. Magufuli amesema kuwa Waziri Mkuu anatajwa kwenye Sheria Na.5 ya mwaka 2015 kuwa ni Mwenyekiti wa Tume hiyo ambapo Wajumbe wake ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Waziri wa Mambo ya Ndani, Waziri wa Elimu ana Mafunzo ya Ufundi, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Waziri wa Fedha na Mipango, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi.

“Nalipongeza sana Bunge la kipindi cha mwaka 2010 – 2015 chini ya Spika mstaafu, Mhe. Anne Makinda lililopitisha Sheria hii baada ya kuona sheria za mwanzo za kupambana na dawa za kulevya hazina nguvu hivyo Wabunge wa wakati ule walisimama kwa pamoja bila kujali itikadi za vyama vyao wakapitisha sheria hii,” alisema Dkt. Magufuli.

Aidha, Dkt. Magufuli amempongeza Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete kwa kusaini sheria hiyo haraka mara baada ya Bunge hilo kuipitisha kwa sababu alijua madhara ya dawa za kulevya katika nchi yetu.

Amefafanua kuwa sheria imeeleza wazi katika kifungu cha 10 cha Sheria Na.5 ya mwaka 2015 kuwa jukumu la kupambana na dawa za kulevya linasimamiwa na Serikali pekee yaani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Makamo wa Rais, Waziri Mkuu, Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na Wilaya pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya au mtu yoyote atakayekuwa amepewa mamlaka ya kusimamia Serikali.

Kwa upande wake Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa amesema kuwa Taifa limeendelea kushuhudia kizazi chetu kikiendelea kudidimia kwa sababu ya matumizi ya dawa za kulevya na Serikali kwa mipango yake imeendelea kukemea, kudhibiti na kuchukua hatua mbalimbali dhidi ya wazalishaji, wasambazaji, wauzaji na watumiaji wa dawa hizo.

“Jambo hili limeleta athari kubwa sana kwani vijana wetu wengi wamepoteza uwezo wa kujisimamia katika shughuli zao za maendeleo kwa sababu baada ya matumizi tumeona athari kadhaa zikiwezo za kudhoofishwa kwa mwili, uwezo wa kutafakari pamoja na kutoweka kwa uwezo wa kufanya kazi,”alisema Waziri Mkuu Majaliwa.

Waziri Mkuu Majaliwa ameongeza kuwa Taifa hili la Watanzania kwa kiasi kikubwa linawategemea vijana waweze kuleta msukumo wa maendeleo ndani ya nchi hivyo jambo hili likiachiwa linaweza kuleta athari kubwa katika ukuaji wa uchumi na maendeleo yetu kwa ujumla wake.

Alisisitiza kuwa vita hii ilianza, inaendelea na itaendelea kupiganwa hadi imalizike hivyo Watanzania hawana budi kuunga mkono jitihada zozote zinazofanywa na Serikali kuhakikisha wanatokomeza uzalishaji, usambazaji, uuzaji na matumizi yake kwa namna yoyote ile, kila mmoja anatakiwa kushiriki kikamilifu ili kubaini matumizi ya dawa za kulevya ndani ya nchi hii.

Read More »

Rais Magufuli Akerwa na Kitendo cha Manji na Gwajima Kwenda na Mashabiki wao Polisi




Inaonyesha kila kinachoendelea huwa kinamfikia Rais Magufuli ambapo leo kwenye hotuba yake IKULU Dar es salaam ameongea kuhusu wale Mashabiki wa Yanga walioonekana kulifutafuta vumbi gari la Mfanyabiashara Yusuph Manji baada ya kuingia kuhojiwa Polisi kwenye sakata la dawa za kulevya.

Pamoja na hilo, rais pia ameongelea ishu ya Wanakwaya wa Askofu Gwajima kwenda na kusimama nje ya kituo cha kati cha Polisi baada ya Askofu huyo kuingia kuhojiwa na Polisi kwenye sakata la dawa za kulevya.

Read More »

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Bandari, Ephraim Mgawe ahukumiwa kwenda Jela miaka mitatu au faini ya Mil.5

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Bandari Ephraim Mgawe ahukumiwa kwenda Jela miaka mitatu au kulipa faini shilingi milioni tano taslimu.


Ephraimu Mgawe na msaidizi wake, walifikishwa katika mahakamani wakikabiliwa na tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka kwa kusaini mkataba wa kuipa kazi kampuni ya ujenzi ya China communications Ltd bila kutangaza zabuni.


Msaidizi wa Mgawe ambaye walifikishwa wote mahakamani hapo ni naibu mkurugenzi mkuu PTA, Amadi Koshuma ambao wote walipandishwa kizimbani mbele ya hakimu mkazi mkuu, mfawidhi, Isaya Arufani katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu, jijini Dar es salaam.

Upande wa jamhuri uliongozwa na wakili wa serikali mkuu, Osward Tibabyekomya akisaidiana na mwendesha mashtaka wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU), Ben Linkolin.

Linkolin alidai kuwa Desemba 5, mwaka 2011 huko TPA, washtakiwa wakiwa waajiriwa wa mamlaka hiyo kwa nyadhifa hizo, walitumia vibaya madaraka yao.

Ilidaiwa kuwa washtakiwa walitumia vibaya madaraka yao baada ya kusaini mkataba kati ya TPA na kampuni ya China communications na kuipa kazi ya ujenzi wa geti namba 13 na 14 ya mamlaka hiyo, bila kutangaza zabuni kinyume cha kifungu cha 31 cha sheria ya manunuzi namba 21 ya mwaka 2004.

Read More »

Nini kinafuata baada ya Freeman Mbowe Kugoma kwenda Polisi Kuitikia Wito wa Makonda? Polisi yatanganza mikakati mizito

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema kama Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe hataripoti bila kutoa taarifa yoyote ya udhuru atafuatwa kwa kuwa jeshi hilo linahitaji  kumhoji.

Kamanda wa kanda hiyo, Simon Sirro amesema hayo leo muda mfupi baada ya Mbowe kueleza kuwa hataripoti polisi kutokana na wito wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Amesema operesheni dhidi ya mihadarati bado inaendelea na kuanzia sasa hawataruhusu tena mkusanyiko wa watu katika kituo cha polisi kati na wale watakaoonekana watashughulikiwa hivyo asije kulalamika mtu kwani taarifa imeshatolewa.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ametangaza rasmi kutofika kituoni hapo kwa madai kuwa hawezi kwenda polisi kwa wito wa Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda isipokuwa pale tu taratibu za kisheria zitakapofuatwa. 

Read More »

Yusuf Manj na Askofu Gwajima Kuendelea Kusota Selo.....Sirro Asema Upelelezi Bado Unaendelea

Kamanda Sirro amesema bado wanamshikilia mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji pamoja Askofu wa kanisa la Ufunuo na Uzima, Josephat Gwajima kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya na upelelezi dhidi yao bado haujakamilika.
Watuhumiwa hao wawili waliripoti kituoni hapo jana mchana na siyo leo kama walivyoagizwa na RC Paul Makonda.
Kamanda Sirro amesema atatoa taarifa Jumatatu kueleza nini kinaendelea kuhusu watuhumiwa hao.

Mpaka wakati anazungumza na waandishi wa habari kamanda huyo alisema walioripoti kituoni hapo ni watuhumiwa 4 kati ya 65 .

Walioshuhudiwa na waandishi wa habari wakiripoti kituoni hapo ni Iddi Azzan, Hussain Pamba Kali pamoja na bosi Sea Cliff.

Read More »

Lissu akiri kutamka, adai hana kosa

Baada ya kukaa mahabusu kwa siku nne, Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amesema kuwa maneno anayoshtakiwa kwa kuyatamka ni ya kweli na kuwa siyo kosa.

Lissu ambaye yupo nje kwa dhamana, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashtaka manne ya kutoa maneno ya uchochezi na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa.

Awali, kabla ya kupandishwa kizimbani mbunge huyo aligoma kula akiwa mahabusu ya polisi kwa mujibu wa wakili wake, Peter Kibatala.

Kutoka kwa Lissu kulifuatia kasoro za kuandaa kiapo kuwa mojawapo wa sababu zilizoifanya Mahakama hiyo kutupa pingamizi la dhamana lililowekwa na upande wa Serikali.

Mbunge huyo amepandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka manne ya kutoa kauli za uchochezi, ambapo upande wa mashtaka uliwasilisha ombi la zuio la dhamana lililoambatana na kiapo cha Mkuu wa Upelelezi wa Polisi Wilaya Ilala, Mrakabu Msaidizi (ASP), Denis Mjumba.

Hata hivyo, mahakama hiyo imetupa pingamizi la dhamana pamoja na mambo mengine kutokana na kasoro katika kiapo hicho.

Akitoa uamuzi wa pingamizi hilo, Hakimu Mkazi, Huruma Shaidi ameainisha mambo matatu yaliyomfanya kulikataa pingamizi hilo na kuamua kumwachia kwa dhamana mtuhumiwa.

Lissu ametimiza masharti hayo na kudhaminiwa na Diwani wa Kata ya Tabata wa chama hicho, Patrick Asenga hivyo akaachiwa huru. #Mwananchi

Read More »

Video..Msukuma Azidi kumwashia Moto Makonda Bungeni,Awaambia Wabunge Wenzake Wamwachie Makonda Apambane Nae Mtaani Ili Amuonyeshe Fresh..!!



Read More »

Mahakama Yatupilia Mbali Pingamizi la Serikali......Yampa Tundu Lissu DHAMANA Ya Milioni 20

Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka manne ya uchochezi.
Wakili wa Serikali Kishenyi Mutalemwa aliwasilisha maombi ya kupinga dhamana yaTundu Lissu kwa madai kwamba amekuwa na mwenendo unaohatarisha amani si tu kwa wanajamii, bali hata kwake mwenyewe kwa kuendelea kutoa maneno ya uchochezi.

Hakimu Huruma Shaidi, ametupilia mbali ombi hilo la serikali na kumpa Tundu Lissu dhamana ya sh. Milioni 20

Read More »

KUMEKUCHA! Makonda Aitwa Bungeni Kujieleza......Ni Baada ya Kutoa Kauli za Dharau Dhidi ya Bunge

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kauli moja limewaita mbele ya Kamati yake ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, na DC wa Arumeru Alexander Mnyeti kwa madai ya kudharau Bunge.

Maamuzi hayo ni sehemu ya maazimio manne ya Bunge yaliyopishwa usiku huu dhidi ya viongozi wanaoteuliwa na Rais hasa wakuu wa mikoa na wilaya, ambapo azimio lingine ni kumtaka Waziri wa TAMISEMI kutoa maelekezo kwa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na kutoingilia majukumu yasiyo yao.

Hatua hiyo inafuatia hoja iliyotolewa bungeni hapo na Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara, kufuatia kauli inayodaiwa kutolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda inayodaiwa kuwa ni dharau kwa Bunge.

Pia Mwita amedai kuwa viongozi mbalimbali hasa wakuu wa mikoa na wkuu wa wilaya wamekuwa wakitumia madaraka yao vibaya kiasi cha kuingilia majukumu yasiyo yao, na wakati mwingine kuingilia majukumu ya Bunge, na kutolea mfano Paul Makonda na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, Alexander Mnyeti.

Baada ya hoja yake kukubaliwa na Mwenyekiti wa kikao hicho Mh Andrew Chenge, wabunge wameijadili ambapo wabunge kadhaa akiwemo Ester Bulaya, Zitto Kabwe, Saed Kubenea na Joseph Musukuma wamepata fursa ya kuchangia ambapo kwa kiasi kikubwa wote wameoneshwa kukerwa na kauli hiyo inayodaiwa kutolewa na Paul Makonda, pamoja na utaratibu wa wabunge kukamatwa bila utaratibu.

Wakati mbunge Zitto Kabwe akipendekeza kuitwa mbele ya kamati viongozi waliotuhumiwa, Ester Bulaya amepasua jipu kwa kusoma ujumbe wa vitisho aliodai umetoka kwa kiongozi mmoja aliyeteuliwa na Rais.

Akichangia mjadala huo, Waziri anayehusika na Bunge pamoja na sera Mh. Jenista Mhagama amewataka wabunge kutomuhusisha Rais Magufuli na makosa yanayofanywa na viongozi aliowateua ambapo amesema kuwa kwa mujibu wa sheria Rais ana majukumu yake, na wakuu wa mikoa na wilaya wana wajibu wao, hivyo kama kuna RC au DC anakwenda kinyume na sheria au kuingilia Bunge, anapaswa kuwajibishwa mwenye.

Baada ya mjadala huo, Chenge amewahoji wabunge wanaokubaliana na mapendekezo ya mtoa hoja, ambapo wabunge wote wameitikia kuunga mkono mapendekezo hayo manne na kuwa maazimio rasmi ya Bunge.

Read More »

Hivi Ndivyo Makonda Alivyozijibu Tuhuma za Wema Sepetu kuwa Anatoka na Agnes Masogange...!!!

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paulo Makonda ametupa jiwe gizani kwa kumjibu Wema Sepetu baada ya siku chache zilizopita kuenea kwa sauti yake mitandaoni akiwa mahabusu huku akimlalamikia mkuu huyo wa mkoa kushindwa kulitaja jina la Agness Masogange kwenye orodha ya kwanza ya watuhumiwa wa madawa ya kulevya.

Akijibu swali kutoka kwa mwandishi wa habari Jumatano hii ofisini kwake wakati akitaja orodha ya pili ya watuhumiwa wa madawa hayo, Makonda amesema, “Ukitaja jina kwanza utakuwa unaingia kama vile unajitahidi kuhama.”

“Hebu wewe kama una taarifa za mitandao sahihi tuambie tu, ndio maana nimesema tunapokea kwa wenyeviti wa mitaa, tunapokea wapi, wewe kama una taarifa sahihi wewe tuambie tu. Lakini usiibue taarifa kwa sababu wewe una jambo la kujibu ukaibua taarifa nyingine tena siyo rasmi, tena nimeeleza hapa ukiwa kwenye mahabusu au popote pale chini ya usimamizi hata simu huruhusiwi kuwa nayo,” ameongeza.

“Kwahiyo bado vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea kucheki pia utaratibu gani uliotumika kwa mtu kujirekodi na kuanza kutoa matangazo wakati upo sehemu sahihi ya kutoa hizo taarifa.”

Majina 65 ya watuhumiwa wa madawa ya kulevya yametajwa kwenye orodha ya awamu ya pili yakiwemo majina makubwa nchini Freeman Aikaely Mbowe, Yusuf Manji, Mchungaji Josephat Gwajima, Iddi Azan na Hussein Pambakali.

Read More »

Kauli ya CHADEMA baada ya Mbowe kutuhumiwa kwa biashara ya dawa za kulevya

Muda mfupi baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutaja orodha ya majina 65 ya watuhumiwa wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeibuka na kukosoa utaratibu unaotumiwa na kuongozi huyo.

CHADEMA kimekosoa utaratibu unaotumiwa wa kutangaza majina hadharani ambapo wamesema kuwa baadhi ya wanaotajwa ni viongozi wa ngazi za juu wa kitaifa.

Mkutano huo ulioongozwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt Vicent Mashinji umekuja saa chache baada ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Aikaeli Mbowe kutajwa miongozi mwa watuhumiwa hao 65.

“Majina mengi yaliyotajwa kuna jina la Mwenyekiti wa chama Mbowe, suala la utetezi wake au maelezo hilo ni suala binafsi sababu kilichotajwa ni jinai lakini kimsingi tunachukua nafasi hii kulaani jinsi tusivyoweza kuendesha utawala wa sheria kwenye nchi yetu na jinsi tusivyofuata kanuni zilizowekwa dhidi ya sheria.

"Mh. Mbowe ni kiongozi wa kitaifa, ni kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, ni Mbunge wa Hai…. kwahiyo kuna taratibu za kufata unapokua na kusudio la kumuita.”

Katibu huyo alisema kuwa si sahihi kutaja majina ya viongozi wakubwa hadharani kwa tuhuma tu ambazo hata hazijathibitishwa. Dkt Mashinji amesema kuwa huko ni kukosa utashi na busara za uongozi.

Katika orodha hiyo ya awamu ya pili iliyotolewa na RC Makonda leo mchana imejumuisha viongozi wengine kama, Askofu Josephat Gwajima, Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, Aliyekuwa Mbunge wa Kinondoni, Iddi Azan


Read More »

Yusuf Manji Aapa Kumshitaki Makonda Kwa Kumchafulia Jina,Kasema Yupo Tayari Kupimwa na Kupekuliwa Kama ni Kweli Anatumia Madawa ya Kulevya

Manji: Nimesikia wakisema natakiwa kufika kituo cha Polisi siku ya Ijumaa.

Manji: Mimi nina nafasi mbili kwenye jamii, Mimi ni mtoto wa baba yangu na nafasi yangu ya pili mimi ni mwenyekiti wa Yanga na nyote mnajua ninavyoheshimiwa.

Manji: Na chaguzi zilizopita mimi nilichukuahukua fomu peke yangu ya kugombea Yanga hivyo naheshimika.

Manji: Huwezi kunitangaza kupitia radio kwamba niende kwenye kutuo cha polisi saa tano. Makonda ni mdogo kwangu kiumri.

Manji: Na katiba inasema kila mtu ana haki yake, Ukinichafua mimi kama Mwenyekiti wa Yanga unachafua Yanga nzima.

Manji: Ukinishutumu mimi ni mpumbavu tu wewe.

Manji: Kama unataka mimi nikusaidie kutaja wauzaji ni kuniweka kwenye hatari.

Manji: Mimi nitaenda Kituo cha Polisi kesho sisubiri hiyo Ijumaa.

Manji: Kifungu cha 66 katika katiba kinaeleze haki zangu na kufungu 32 pia. Vinanilinda.

Manji: Nataka nimshitaki Mahakamani na vyombo vyote vilivyoandika kunituhumu na madawa.

Manji: Kesho naenda Polisi asubuhi nihojiwe baada ya hapo naanza kutafuta haki yangu. Huwezi kuniita kaka huku unanitaja kwenye mambo mabaya.

Manji: Wapo watu kwenye mtandao wameanza kuandika vitu, Alichofanya mkuu wa mkoa ni kosa siwezi kukubali.

Manji: Na Wanayanga kama mnaona mimi sifai na kama hamna imani na mimi hata kesho naondoka Yanga. Siwezi kuchafua Club kubwa.

Manji: Kwanini RC Makonda hajamuita Askofu Pengo au Mashehe wamsaidie?

Manji: Hiwezi kuniita mimi kama mbwa njoo, Hii ni kutafuta masifa. Kesho utanikuta mimi kwenye gazeti na wengine 65 watasahaulika. Hii sio haki.

Manji: Zipo njia za kushughulikia vitu, Tukienda Comoro tunaenda na bendera ya Tanzania.

Manji: Kama unataka msaada omba msaasa sio unaagiza msaada, Unaniita na watu 65 nikae kwenye foleni, watu 65 watamaliza saa ngapi? Saa tano usiku nitoke? Sina kazi nyingine za kifanya?

Manji: Yupo mzee mmoja na wenyewe mnamjua, alinitukana nikamdai shilling moja. Unanihusisha mimi jina langu nloachiwa na baba kwenye huu upumbavu halafu unathubutu kiniita kaka yako?

Manji: Hii itanifanya nishindwe kwenda Comoro na Klabu ya Yanga sababu Wanacomoro watasema nimepeleka madawa. Wananichafua sana.

Manji: Hivi ni vita na wanahitaji msaada haraka na kama wana shutuma au ushahidi au huo msaada wanieleze. Kama vita kwanini isiwe leo wasubiri ijumaa. Mimi naenda kesho.

Manji: Kesho nyie watu wa magazeti na habari msitoe habari kwa upande mmoja.

Manji: Ambao hawatabalance habari. Cybercrime inasema ukiweka habari ya uongo unafungwa. "Ambaye ataandika makonda manji dawa za kulevya" kesho namshitaki.

Manji: Wakina Amina Chifupa walitaja majina, yalienda wapi? Hii jitihada hakuna mtu anakataa. Hata unayemchunguza humtaji kwenye vyombo vya habari. Hata TAKUKURU hawawataji wanaowachunguza. Mimi siwezi kwenda kutaja mshahara wa mfanyakazi. Nitakiwa namvunjia heshima.

Manji: Mimi nipo tayari kupimwa na kusearchiwa na Makonda naye apimwe kama anatumia na wamsearch pia.

Manji: Mimi sitaki kuchanganya vitu viwili kwenye mkutano mmoja. Kesho au keshokutwa ntafanya mkutano kuanzia PSPF, Coco Beach nk. Leo nakaa kwenye point moja tu ya madawa.

Manji: Mkuu wa mkoa kunasehemu nimegongana naye oysterbay na nlienda kuonanana naye kama diwani wa mbagala kuu kumuomba mkuu wa majeshi atakayekuja ahamishe kambi ya jeshi kutoka mbagala na kupelekwa nje ya mji. Kama diwani siwezi kumuandikia rais.

Read More »