Kauli ya CHADEMA baada ya Mbowe kutuhumiwa kwa biashara ya dawa za kulevya

Muda mfupi baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutaja orodha ya majina 65 ya watuhumiwa wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeibuka na kukosoa utaratibu unaotumiwa na kuongozi huyo.

CHADEMA kimekosoa utaratibu unaotumiwa wa kutangaza majina hadharani ambapo wamesema kuwa baadhi ya wanaotajwa ni viongozi wa ngazi za juu wa kitaifa.

Mkutano huo ulioongozwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt Vicent Mashinji umekuja saa chache baada ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Aikaeli Mbowe kutajwa miongozi mwa watuhumiwa hao 65.

“Majina mengi yaliyotajwa kuna jina la Mwenyekiti wa chama Mbowe, suala la utetezi wake au maelezo hilo ni suala binafsi sababu kilichotajwa ni jinai lakini kimsingi tunachukua nafasi hii kulaani jinsi tusivyoweza kuendesha utawala wa sheria kwenye nchi yetu na jinsi tusivyofuata kanuni zilizowekwa dhidi ya sheria.

"Mh. Mbowe ni kiongozi wa kitaifa, ni kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, ni Mbunge wa Hai…. kwahiyo kuna taratibu za kufata unapokua na kusudio la kumuita.”

Katibu huyo alisema kuwa si sahihi kutaja majina ya viongozi wakubwa hadharani kwa tuhuma tu ambazo hata hazijathibitishwa. Dkt Mashinji amesema kuwa huko ni kukosa utashi na busara za uongozi.

Katika orodha hiyo ya awamu ya pili iliyotolewa na RC Makonda leo mchana imejumuisha viongozi wengine kama, Askofu Josephat Gwajima, Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, Aliyekuwa Mbunge wa Kinondoni, Iddi Azan