HUYU NDO MSANII WA TANZANIA ANAYEJIITA MUNGU WA BONGO FLEVA>>>

Kwenye sanaa ya muziki imezoeleka kuwa kila msanii ana jina lake alilopewa na wazazi wake pamoja na jina lingine ambalo atajiita mwenyewe kutokana na kile anacho kifanya.
Msanii wa nyimbo za bongo fleva Q Chief amesema yeye ni ‘Mungu’ wa bongo fleva jina ambalo amepewa na mashabiki wake.

Amesema amelipokea jina hilo kwa kuwa anaamini kwamba kweli yeye ni ‘Mungu’ wa bongo fleva kupitia nyimbo zake.
Q Chief amesema wapo ma’simba na wafalme lakini mashabiki wake wameamua kumuita jina hilo na anajivunia kwa kazi zake ambazo wadau wake wamekuwa wakizipokea kwa furaha.
eatv.tv