Miujiza ya mihogo mibichi na nazi Mbata kwa wanaume ,soma zaidi hapa

Kwa mujibu wa uchunguzi huo, imebainika kuwa uwezo wa mihogo na nazi mbata katika kuwasaidia wanaume kwenye ushiriki wa tendo la ndoa hutokana na wingi wa virutubisho vilivyomo, hasa madini ya Zink na Potassium (kwenye mihogo mibichi) na kiambatana cha selenium kinachopatikana kwenye nazi mbata.

Mtaalamu mmoja wa masuala ya lishe jijini Dar es salaam aliiambia Nipashe……..>>>’Vyakula hivi vina maajabu makubwa kwa afya ya akina baba, vinapoliwa kila mara na tena kwa kuzingatia usafi, huwasaidia wengi katika kuimarishha nguvu zao za tendo la ndoa na hivyo kuwapa heshima kwa wenza wao‘ 
Ofisa utafiti wa Taasisi ya chakula na Lishe Tanzania, Walbert Mgeni alisema mihogo mibichi na nazi kavu (mbata) ni vyakula ambavyo vimethibitishwa kitaalam kuwa husaidia kuimarisha nguvu za tendo la ndoa kutokana na madini mbalimbali yanayotokana hasa na Zinc.
Alisema kwa sababu hiyo ndiyo maana kuna kina baba wengi hutumia bidhaa hizo jijini Dar es salaam na kwengineko nchini huku wauzaji wake wakubwa wakiwa akina mama.  
SOURCE: NIPASHE