Vanessa Mdee asema hana Haraka ya Kupata Mtoto na Jux



Msanii wa muziki wa kizazi kipya Vanessa Mdee amefunguka na kuweka wazi kuwa kwa sasa hana haraka ya kupata mtoto na mpenzi wake Juma Jux na kwamba kwa sasa watoto wapo wengi wa kuwalea.

Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Televison Vanessa Mdee amedai kuwa hana haraka ya kupata mtoto na mpenzi wake Jux na kudai kwa sasa wapo watoto wengi wa kulea akiwepo mtoto wa Diamond Platnumz, mtoto wa Shetta pamoja na mtoto wa mtangazaji wa kipindi cha Planet Bongo Dullah Mjukuu wa Ambua kwani wote hao ni kama watoto wake.

“Kiukweli sina haraka ya kupata mtoto na Jux kwani saizi bado kuna watoto wengi wa kuwalea kama mtoto wa Diamond, Shettah na mtoto wako Dullah kwani wote hao kwangu ni kama wanangu tu” alisema Vanessa

Mbali na hilo Vanessa Mdee alisema kuwa mara nyingi anajitahidi kufanya media tour katika nchi za watu kutokana na ukweli kwamba watu wa nje ni wazito sana kupokea kazi za wasanii ambao siyo wao.

“Unajua nafanya sana media ‘tour’ kwani wenzetu ni wazito sana kupokea kazi za wasanii wa nje ya kwao, hivyo hizo media tour zinanisaidia kujenga Fan Base katika nchi zao, kuongeza mzunguko wa kazi zangu kuchezwa kwao, hata kutafuta mashavu mengine” alisema Vanessa Mdee