RAIA MWEMA : BENKI ZAKUMBWA NA UKATA MKUBWA

Wakopaji kutoka sekta mbalimbali za uchumi huenda wakakabiliwa na changamoto za ukosefu wa fedha au kukumbana na viwango vikubwa vya riba sasa na baadaye, kutokana sekta ya benki kukabiliwa na uhaba wa fedhaa benki
Hii ni habari katika ukurasa wa mbele wa gazeti la Raia Mwema la siku ya leo huku habari hiyo ikiwa ndio habari kuu.

Hali hii pia itasababisha wakopaji wengi kupewa kupewa na masharti magumu ya kupata mikopo kwenye benki za biashara hasa kipindi hiki ambacho adadi ya mikopo kichefuchefu (mikopo ambayo imeshindikana kulipa) imekuwa chngamoto kubwa.

Kwa mujibu wa ripoti za Benki Kuu BoT kiwango cha mikopo kichefuchefu ni zaidi ya asilimia tano, ambacho ndicho kiwango cha wastani.
Hadi kufikia mwezi Juni mwaka huu, Mikopo kichefuchefu iliongezeka hadi kafikia asilimia 8.3 kutokaasilimia 6.7 mwezi Machi mwaka jana.

Kuongezeka kwa mikopo kichefuchefu ni ishara mbaya kwani huashiria kupungua kwa imani ya wateja dhidi ya benki. Ukata huo ambao tayari umeonekana kwenye soko, umesababisha kuongezeka cha riba ambacho benki hutumia kuikopesha benki nyingine kwani mahitaji ya fedha kwa ajili ya benki kuyafanyia biashara yamekua kwa kwasi.

Kwa mujibu wa ripoti za fedha za BoT, kiwango cha riba ya mikopo baina ya benki kiliongezeka hadi kufikia wastani wa asilimia 18 hadi Jumatatu wiki hii.
Ripoti hiyo inaonyesha kwamba viwango vya riba ya jumla kwa mikopo baina ya benki kiliongezeka na kufikia asilimia12.31 kutoka asilimia 11.17 huku riba ya ya mikopo ya siku moja kiongezeka hadi asilimia 12.25 kutoka asilimia 11.6

Kwa mujibu wa mapitio ya ripoti ya uchumi mwezi Juni mwaka huu, benki zilikopeshana kiasi cha shilingi trilion 1.28 kutoka shilingi 1.12 mwezi Aprili mwaka huu. Ukubwa wa kiwango hiki cha mikopo baina ya benki huakisi pia viwango vya mikopo ambayo benki hizo hutoa kwenye sekta za uzalishaji mali pamoja na mikopo ya biashara.

Chanzo: Kutoka magazetini.