Fahamu Mengi kuhusu Ugonjwa wa Malaria
Malaria ni nini? Malaria ni ugonjwa wa kuambukizana unaoletwa na chembe chembe zinazoitwa plasmodium.Chembe chembe hizi huingia ndani ya mwili wa binadamu baada ya kuumwa na mbu wa kike kwa jina Anopheles. Mbu mwenye chembe chembe za plasmodium anapomuuma mtu,humuingizia baadhi ya mate yenye viini vya kuambukizana kwenye kidonda hivyo kusabaza Malaria. Viini hivi husafiri hadi kwenye maini ambapo hukaa hadi vifikie ukomavu. Viini hivi baadaye huingia na mtu kama huyu akiumwa na mbu,mbu huyu hubeba chembe chembe hizi na anaweza kumuambukiza mtu atakaye muuma.
Kuna aina 4 za Malaria: P. vivax, P. malariae, P. ovale na P. falciparum. Zimepewa majina kulingana na aina ya plasmodium inayozisababisha. Aina 3 za kwanza sio hatari lakini Falciparumni hatari sana na hata inaweza kusababisha kifo. Hii ni kwa sababu ikishaingia tu mwilini huzaana kwa wingi ndani ya damu.. Hii ni kwa sababu chembe chembe nyekundu za damu(ambazo husambaza oksijeni mwilini)zilizoadhirika huwa nzito na haziwezi kuingia kwenye kapilari. Hii husababisha kufa kwa sehemu ya ubongo,maini,mapafu,figo na matumbo kwa sababu ya ukosefu wa oksijeni. Hali hii inaweza kusababisha kifo kama haita tibiwa haraka.
Malaria hutambulika vipi?
Baridi,kuuma kwa misuli na kichwa zinaweza kuwa dalili za magonjwa mengi mengine. Njia ya pekee unayoweza kudhihirisha kama una Malaria ni kuenda hiospitalini kupimwa damu. Watu wengi wanaotoka sehemu zilizoadhirika na Malaria pindi wanapoona dalili hizi huenda kwenye maduka ya kuuza madawa kununua dawa za kupambana na Malaria. Huu sio ushauri mzuri. Ni muhimu kupimwa damu ili aina ya plasmodium inayosababisha maradhi yako itambulike na upewe matibabu yanayostahili.
Nani yuko kwenye hatari ya kuambukizwa Malaria?
Watoto wachanga,watoto na akina mama waja wazito wako kwenye hatarikubwa ya kushambuliwa hata kufa kutokana na Malaria. Watoto wachanga na watoto wako kwenye hatari kwa sababu wameambukizwa mara chache nahawajajenga
kinga dhidi ya chembechembe hiziVamizi la Malaria kwa wanawake wajawazito kalikwa sababu kinga yao dhidi ya maradhi huwa chini wakati wa uja uzito. Malaria huongeza tishio kwa mtoto ambaye hajazaliwa kama kuzaliwa kabla ya wakati
kutimia, uaviaji wa mimba, maambukizi ya sehemu za siri, uzani mdogo wa mtoto anapozaliwa, kupoteza uja uzito na pia ugonjwa huu unaweza kumsababishia mama kifo.
Naweza jilinda vipi dhidi ya Malaria?
Msafiri: Kama unasafiri hadi kwenye eneo linalolotambulika kwa Malaria,mtembelee daktari wako ili akupe dawa mahsusi ya kupambana na Malaria ya eneo unalotembelea.Hakikisha umefuata maelezo vizuri.
Wenyeji wa maeneo yalioadhirika na Malaria: Mbu wa aina ya anopheles hupenda kuuma watu nyakati za macheo na machweo kwa hivyo ni bora kujikinga nyakati hizi.Wakati wa machweo unaweza keti ndani ya nyumba iliyoekewa dawa na usiku unaweza kulala neti iliyotibiwa.
Haribu sehemu mbu wanapozaliana: Kipindi cha mwisho katika ukuaji wa mbu hufanyika majini.Mbu wa aina ya anopheles hupendelea maji yasiyo ya chumvi.Ni muhimu kuharibu ama kunyunyuzia na dawa sehemu zote ambazo mbu wanaweza kutaga mayai.Unafaa kutoa chupa,ndoo ama chochote ambacho kinaweza kusimamisha maji,bacillus thuringiensis(Bti) dawa asili ya kuua wadudu kutoka BioVision inaweza kutumiwa kuua mbu wachanga bila kuharibu maji.
Watoto na mama waja wazito lazima wakingwe na Malaria: Nchini Kenya,wanawake waja wazito wana haki ya kupata matibabu 2 ya bure na neti zilizotibiwa. Chukua moja kutoka katiki kliniki yako.
Neti zilizotibiwa: Kila mtu anapaswa kupata neti iliyotibiwa.Kuna aina mbili ya neti hizi nchini Kenya ambazo zinauwa mbu pindi tu wadudu hawa wanapozigusa.Kuna zile zinazopaswa kutibiwa kila baada ya miezi 6nba PowerTabs na zile zinazodumukwa miaka 3 hadi 5 baada ya kutibiwa
Ni zipi dalili za Malaria?
Dalili za Malaria ni kama zile za Flu; homa, baridi na kuuma kwa misuli na kichwa. Watu wengine hupatwa na kichefuchefu, kutapika na kuharisha. Vipindi vya baridi, homa na kutokwa na jasho hujirudia kila siku moja, mbili au tatu. Watu wenye aina ya P. falciparumwanaweza kupata Malaria ya ubongo ambayo husababisha kuishiwa na fahamu ama kuchanganyikiwa kiakili.
Tiba ya Malaria
Tiba ya Malaria inategemea mambo kadhaa:
Hali ya mgonjwa (mtoto, mama mja mzito, mtu mzima, ni kali ama sio kali)
Nguvu ya dawa dhidi ya ambukizo la viini vya plasmodium.
Eneo la kijiografia ambalo mtu aliambukizwa. Kwa mfano, P.falciparuminayopatikana katika nchi za Mashariki ya kati inaweza kutibiwa na dawa ya chloroquine, lakini inayopatikana Africa, katika nchi zilizo kusini mwa jangwa la Sahara haitibiki kwachloroquine.
Aina ya plasmodium inayodhuru mgonjwa. Malaria yasiyo makali hutibiwa na dawa za kumeza ilhali wagonjwa wenye P. falciparum kali hulazwa hospitalini na kupewa sindano ya maji.