Rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud anasema anawataka Wasomali vijana waliopo nje ya nchi kurejea nyumbani.
Rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud anasema anawataka Wasomali zaidi vijana waliopo nje ya nchi kurejea nyumbani.
Kurejea kwao ni kusaidia kuijenga nchi licha ya kwamba wanamgambo wa Al-Shabab wanaendelea na mashambulizi hatari.
Rais Mohamud aliongea na VOA mjini Mogadishu na kujibu maswali kuhusu masuala mbalimbali katika mkutano uliofadhiliwa na VOA siku ya Jumamosi.
Tukio hilo lilikuwa la kwanza la kipekee kuunganisha Mogadishu mji mkuu wa Somalia, na mji wa St. Paul, jimboni Minessota, ambapo kuna jumuiya kubwa zaidi ya Wasomali nchini Marekani.
Rais huyo alisema Wasomali waliopo nje ya nchi wamehusika katika mfumuko wa biashara nyingi nchini hasa mji mkuu wa Somalia, toka kuondoka kwa kundi la Al-Shabab mji humo mwaka 2011.