Dalili ambazo zitakuonyesha kwamba ukaribu wako na huyo rafiki utakupelekea kuisaliti ndoa yako au Mahusiano yako
Dalili ambazo zitakuonyesha kwamba ukaribu wako na huyo rafiki utakupelekea kuisaliti ndoa yako au Mahusiano yako, soma hapa
2. Unajikuta ukichagua mavazi na kujikagua sana ukijiuliza jinsi atakavyo vutiwa na mavazi yako pale atakapokuona
3. Unapokuwa naye unajikuta ukimweleza matatizo ya mahusiano yako na mpenzi wako au mumeo
4. Unajikuta ukimgusa gusa wakati mkiongea au kufanya naye utani unaoweza kupeleka ujumbe tofauti kwake kwamba labda umevutiwa naye kimapenzi.
5. Unawsiliana naye kwanza kabla ya kuwasiliana na mpenzi wako au mumeo pale unapokabiliwa na jambo lolote lenye kutatiza na linalohitaji msaada wa haraka au ushauri
6. Unajikuta ukiwaza jinsi gani ungekuwa na amani iwapo ungekuwa na uhusiano naye wa kimapenzi au ndoa
7. Inawezekana ukawa unamzuingumzia sana kwa mwenzi wako au kwa marafiki zako, au inawezekana ukawa humzungumzii kabisaaa na kuficha urafiki wenu.
8. Unajitahidi sana kuficha urafiki wenu na kutomzunguimzia rafiki huyo kwa mwenzi wako kwa sababu unajua kwamba jambo hilo linaweza kukuletea balaa.
Kwa ujumla unapojikuta umempata rafiki mwenye jinsia tofauti na yako halafu ukahisi kulipukwa na moyo juu yake zikiwemo dalili nilizozitaja hapo juu, basi ujue uhusiano wako na mume au mpenzi wako uko mashakani. Usipokuwa makini utamsaliti.