Kuna Mapenzi ya kweli kati yako na Mpenzi wako? ,Unahisi unapendwa? Makala ya Mapenzi Matamu

Upo kwenye mahusiano ya Kimapenzi? Unahisi unapendwa na mpenzi wako? Haya ni mwaswali ya kujiuliza kuelewa hii Makala.

Katika mahusiano wengi kama si wote hupenda kuelewa mpenzi wake anampenda kiasi kipi, pengine saa ingine hata kutamani angekuwa na uwezo wa kuona nafsi ya mpenzi wake huyo ni kwa kiasi kipi penzi hilo limetawala; bahati mbaya ama nzuri haiwezekani.  Hata hivyo kuna dalili katika mahusiano kati ya wawili ambazo uashiria endapo mpenzi wako huyo anakupenda ama lah. Hii huambatana na kutokana na tabia na nyenendo za mpenzi wako huyo dhidi yako.
Baadhi ya viashiria ambavyo vinaweza kukusaidia katika kutafakari ama kutambua endapo Mpenzi wako huyo ni kweli anakupenda.
Mawasiliano egemezi kati yenu (Communication)
Hii ni mawasiliano kwa njia za viwezesha mawasiliano hasa simu. Sasa hivi mawasiliano yamerahisishwa mno ikiwa na njia nyingi kama vile kupiga simu, njia za messages hasa kama vile Whatsapp, Viber, Skype na text messages. Kwa yeyote aliye na simu ya mkononi ni rahisi kuwasiliana na mpenziwe wakati wowote ule. Mawasiliano ni njia moja wapo ya muhimu sana katika kujenga na kuboresha mawasiliano kati ya wapenzi. Inapotokea mawasiliano hayo yame elemea Zaidi upande mmoja siku zote; hapo kidogo ni tatizo. Kimsingi mawasiliano hupaswa kuwiana (mtu na mpenzi wake wote watafutane kwa usawa) ingawa inaweza pishana kidogo tokana na sababu mbali mbali. Ila inapotokea siku zote mpenzi wako huyo katka mawasiliano hufanya haya;
–          Hakutafuti siku zote hadi uanze wewe.
–          Kukukatia simu na kukuzimia bila maelezo yoyote ya msingi.
–          Kuwa mkali kila ukimtafuta, kukuonyesha kana kwamba simu zako kwake ni kero.
–          Kuchukua mda mrefu kujibu jumbe zako ama kutojibu kabisa na hata ukimuuliza hakuna sababu za msingi.
*Kwa baadhi ya tabia hizo katika mawasiliano ni dalili ambazo zinachangia kuonyesha kuwa mpenzi wako huyo hakupendi. Na hasa ikiwa tabia hizo zote anazo zote.
 Ushirikiano egemezi kati yenu
Ushirikiano ni muhimu baina ya wapenzi katika masuala yale ambayo ni msingi katika maisha yenu; kila mmoja anapaswa kushiriki na kujitoa kwa mpenzi wake kwa yale yote ambayo huitaji ushiriki kwa mpenziwe. Ushirikiano hu upo wa aina mbili.
Kuna ushirikiano wa hali:-
Ushirikiano huu ni namna ambavyo wewe na mpenzi wako hushirikiana hasa katika mambo ya kijamii, kijamaa, kifamilia nakadhalika; ya wale na vile vilivyokuzunguka. Ikiwa pale unapokua na tatizo kama vile kuugua/kuuguliwa,  misiba ama matatizo mengine yoyote yeye siku zote ana sababu za kushindwa kuwa karibu yako. Na ikitokea akapata nafasi yupo juu juu akionyesha dalili za kutokua comfortable kua hapo.
Kuna ushirikiano wa Mali:-
Ushirikiano huu ni namna ambavyo wewe na mpenzi wako hushirikiana linapokuja suala la kujitoa kwa vitu vihusuvo pesa bila kujalisha kipato cha mwenzako. Ikiwa una mpenzi wako akawa na shida ama kuhitaji msaada wa kifedha ama unaohususha matumizi ya fedha (bila kujalisha ni mwanamke ama mwanaume) huwa ni muhimu kutoa msaada huo; hasa pale ambapo ni wazi kabisa mwenzio anakuwa amekwama.  Kuna baadhi ya wapenzi hawezi toa msaada wa mali hata kidogo; ingawa naamini kuwa mtu yeyote yule anapokua na mtu anampenda sana ni lazima atataka kumsaidia mwenzie wakati wa shida.

Taratibu za kuonana (Meetings)
Katika hiki kipengele cha Kuonana kipo katika maeneo mawili pia.
Nafasi yake ya kukuona:- 
Mtu yeyote hata kama yupo na majukumu kiasi kipi, akimpenda mwenzie (iwe kwa mwanamke ama mwanaume) atatafuta tu muda  kwa ajili ya kuwa na mpenzi wake. Haijalishi huo muda utakua mfupi ama mrefu, dakika chache ama masaa, ila tu lile wazo la kutomuona mpenzi wake kwa muda mrefu na hali yupo karibu na ana uweo huo linamkosesha raha. Ikiwa mpenzi wako yupo karibu, na unajua fika anauwezo wa kukuona na kuwa na wewe mara kwa mara lakini haipo hivyo – hiyo inaweza kuwa moja  ya dalili ya kutopendwa na huyo mtu (labda kuwe na sababu za msingi na iwe ni kitu cha kupita na si tabia yake).
Maeneo ya kuonana:-
Hii inahusu mpenzi wako kutotaka ufike kwake (na hali pengine anakaa peke yake ama yeye ndiye mmiliki wa anapoishi). Siku zote atataka aje kwako ama mkutane sehemu za maficho. Pia linahusu yeye kutotaka kuonekana na wewe kwa watu ama katika jamii. Yupo radhi siku zote mkutane mahala na kila mmoja aondoke vyake, ama kama ana usafiri akuchukue toka utokapo hadi pale mnapoelekea.
Kutokuwa na chembe ya Wivu dhidi yako
Wivu ni kiungo muhimu sana katika mahusiano, mwanadamu hachagui ni wakati upi awe ama asiwe na wivu, hilo lipo ndani yetu na ni kitu ambacho hakizuiliki ikiwa kweli mtu wako wampenda. Kinachotutofautisha wote ni viwango vya wivu na namna/wapi wa kuonyesha huo wivu. Wivu haimaanishi kuwa mtu hajiamini ama kuwa ndio hampendi mwenza wake; wivu huja ‘naturally’ mana unapo mpenda mwenzako kiukweli kwa ni wazi kua mapenzi ya kweli ya viwango vya wivu ndani yake na  kutaka chako kiwe chako peke yako na  hivyo kutaka kukilinda chako kubaki chako siku zote.
Inaptokea mpenzi wako hana habari kabisa, na wala hashtuki ni wazi kuwa anaweza kuwa asiwe anakupenda vile ambavyo mhusika ungetaka. Ikiwa yeye haisumbui kabisa ukiwa na wengine, akikukuta na wengine, akihisi upo  na wengine hapo ni wazi kuwa hakuna mapenzi yale ya dhati.
Hata hivyo ni muhimu sana kutoendekeza wivu katika mapenzi na kuwa makini kiasi cha wivu dhidi ya mpenzio. Wivu kwa kiwango ni chachu katika mapenzi, Wivu uliokithiri huwa kero tokana na tabia ambazo huambatana na wivu huo ambao mwisho wa siku huwa karaha na kero katika mahusiano.
Kutokutambulisha kwa Ndugu, Jamaa & Rafiki
Kawaida wengi wa wenye wapenzi ambao haswa wanawapenda, hutaka ndugu, jamaa na marafiki zao wawajue na mara nyingi hata kutambulisha kabisa kuwa ni mtu wake. Ikiwa upo katika mahusiano na mtu wako hapendi kukutambulisha kwa watu wake wowote katika maisha yake hilo nalo linaweza kuwa ni tatizo. Ingawa wengi huwa rahisi kukutambulisha kwa marafiki maana yeye pamoja na marafiki zake hujuana kwa viremba.
Sababu za Kukutafuta zinamhusu yeye tu (Selfish reasons of Meetings)
Kila akikutafuta anakutafuta sababu tu anashida toka kwako.
Kwa wanawake mara nyingi inaweza kuwa anashida toka kwako ya kitu Fulani, ama kufanyiwa kitu Fulani ama shida ya pesa. Nje ya hapo hahawahi kukutafuta kwa sababu tu kakukumbuka, ama sababu tu anataka kupumzika na wewe ama sababu yoyoye ile ambayo haimnufaishi yeye tu.  Wapo na wanaume ambao pia wana wapenzi wao wanawatumia na kila wakiwatafuta inakuwa ni sababu tu wanataka kitu ama fedha toka kwa wapenzi wao.
Kwa wanaume hii mara nyingi huwa shida yake kubwa kwako ya kuonana ni kutaka kukutana kimwili. Na akishamaliza hapo basi kuonana ni tatizo hadi pale tena atakapotaka kukutana na wewe kimwili.
Anavyokuita hasa majina mbadala (The way they address you)
Hii inahusu namna atakavyo kuita mkiwa wenyewe ama mbele za watu. Kuna watu wasio na haya na ukimchekea anaweza hata muita mpenzi wake mbele yake na hata kwa wenzie majina kama demu (kwa mwanamke) ama buzi langu (kwa wanaume). Hii ni mifano tu, kuna aina ya majina mengi ambayo si busara kuyatumia, na ambayo naamini mtu ambaye anampenda na kumthamini mpenzi wake hawezi yatumia iwe yupo na mpenzi wake ama hayupo na huyo mpenzi wake.
Namna anavyo Kuthamini/Kujali/Kuheshimu
Ikiwa mpenzi wako hakujali, hakuheshimu, hakusikilizi, hakuweki kipau mblele pale panapostahili ina maana kuwa hakuthamini. Kuthamini huja tu pale ambapo kuna mapenzi ya kweli dhidi ya mtu wako. Ni kitu ambacho huwezi kulazimisha, na hata ukilazimisha kwa siku chache mwisho wa siku mhusika atachoka kujifanya anakuthamini na hali hakutamini. Thamini inatokana na neon thamani… Kile kilicho na thamani siku zote mtu kukitunza kwa uangalifu, upendo na kujali kwa hali ya juu sana.  Mtu anaye kuthamini ni lazima atakuheshimu na kukukali, ila si lazima kuwa mtu anaye kujali na kukuheshimu atakuthamini. Mpenzi wako akikuthamini, siku zote atakua karibu na wewe, atajali hisia zako, atajali afya yako na atajali yote yale ambayo ni msingi kwako na wale wote waliomzunguka.
Tendo la ndoa (Sex)
Hili la tendo la ndoa linaweza kutazamwa kwa namna mbili
*Ikiwa hashirikiani na wewe kwa lolote lile (hali na mali), hakuthamini na tabia zote ambazo huonyesha kutofurahia kuwa na wewe wakati wowote ziku zote LAKINI linapokuja suala la kukutana kimwili ndio hulipa kipaumbele. Hapo ni tatizo. Inakuwa ni wazi hukuhitaji tu kwa sababu ya kukidhi haja zake za kimwili.
*Ikiwa hashirikiani na wewe kwa lolote lile (hali na mali), haonyeshi kuthamini na tabia zote ambazo huonyesha kutofurahia hayo mahusiano hasa kama pia ana tabia ya kukutafuta tu pale ambapo yeye ana shida; inapotokea ukitaka kukutana nae kimwili anasita/hapendi/hafurahii ama kutokua na ushirikiano mzuri katika tendo – hapo ni wazi pia kuwa hakupendi ila anakutumia tu.
MSOMAJI NAOMBA ZINGATIA
Mawazo yangu ya nakala hii ni muhimu sana na ina nguvu Zaidi kwa wale ambao wapo katka mahusiano kati ya wawili. Kwa maneno mengine, ikiwa upo katika mahusiano ambayo unajua kabisa kuwa nyie kama wapenzi wa huyo mpenzi wako mpo Zaidi ya mmoja kuna masuala ambayo yametajwa hapa na hayawezi tumika kama kigezo cha kuelewa endapo mpenzi wako huyo ni kweli anakupenda ama lah.
 Ikiwa unahisi mpenzi wako hakupendi, hiyo si lazima ikawa ticket ya maamuzi ya kusonga mbele. Unaweza chukua baadhi ya hatua ili kuboresha hayo mahusiano na yakaenda kwa mtindo ambao wote wawili mnaweza yafurahia. Ikumbukwe kuwa kila mmoja anapo ingia katika mahusiano huingia na mtu mwenye tabia mpya, jamii iliyomsunguka mpya na kadhalika; na hivyo kuanza upya kuyajenga mahusiano mengine. Hivyo ni bora ukajitahidi kurekebisha ulipo (hasa kama kweli unampenda) na pale inaposhindikana yapaswa ukubali na kusonga mbele.