DIAMOND AFUNGUKA KUHUSU COLLABO YAKE NA LADY JAY DEE



Baada ya kilio cha muda mrefu kutoka kwa mashabiki waliotamani kuona Diamond Platnumz na mwanadada Lady Jay Dee wakifanya kazi pamoja, wakali hao wa bongo fleva huenda wakaja na ‘collabo’ ya hatari, siku chache zijazo.

Hatua hiyo inatokana na msanii Diamond kufunguka kuwa hakuna sababu yoyote inayowakwamisha kufanya kazi ya pamoja, isipokuwa muda na ratiba zao kubana.

Dangote ametoa kauli hiyo hivi karibuni alipotembelea ofisi za EATV, na kukutana na maswali mbalimbali ikiwemo sababu za wao kutofanya kazi ya pamoja licha ya mashabiki kuitamani ‘collabo yao.

“Siku si nyingi tutafanya kazi pamoja na Jay Dee, kilichotukwamisha ni ratiba zetu, lakini pia nilikuwa sijafikiria hilo, ila sasa kwa kuwa mashabiki wamekuwa wakiomba kila mara, nitawasiliana naye, na tutafanya kazi ya pamoja muda mfupi ujao, hakuna sababu nyingine tofauti na kubanwa na kazi nyingi, pamoja na ratiba zetu kutoendana”

Kuhusu ni lini mashabiki wategemee kazi hiyo, Dangote alisema kuwa hawezi kuahidi tarehe, lakini ana uhakika ‘collabo’ hiyo inakuja.

eatv.tv