ZINGATIA MAMBO HAYA YATAKUWEKA KARIBU NA NDOA YAKO

1. MUOMBEE
Hili sio tu kwamba litakukumbusha kuhusu mema ya Mungu kwako, bali pia itakufanya uyajua mahitaji ya mumeo ya siku hiyo na kumuombea ili afanikiwe katika mahitaji yake.

2. DAIMA MBUSU MNAPOKUTANA NA KUAGANA
Huu ni ukaribu wa kimwili na kihisia ambao huwakumbusha mume na mke kuhusu ndoa na muungano wao. Lifanye hilo kuwa mazoea yako ya kila siku, unapoondoka mbusu, unaporudi mbusu tena.

3. MPIGIE AU MUANDIKIE UJUMBE MFUPI WA SIMU ANGALAU MARA MOJA KWA SIKU
Mnaweza kupeana taarifa namna siku inavyokwenda. Mnaweza kujadili kuhusu mahitaji yoyote wakati wa jioni na kuhakikisha kuwa kila mmoja wenu amejumuishwa katika mikakati yenu.

4. ANGALAU DAKIKA 5 ZA MAZUNGUMZO HURU
Iwe asubuhi au usiku, daima mahusiano yoyote yanahitaji mazungumzo. Zimeni televisheni, zimeni simu zenu na mzungumze. Linaweza kuwa gumu, hasa mkiwa na watoto wadogo, lakini tafuta namna ya kulifanikisha hilo. Kama ukiwa na jambo lako unapata muda wa kulifanya bila kujali upo ‘bize’ kiasi gani, kwa nini usipate muda kwa ajili ya mwenza wako?

5. MKUMBATIE ANGALAU KWA SEKUNDE 30
Kabla hujaelekea kazini au unaporejea nyumbani au unapoelekea kitandani, mbusu mwenza wako, kwa maana jambo hilo litawapa hisia tamu na maridhawa za kimwili, kiroho na kiakili. Tafiti mbalimbali zimeonesha kuwa kumbatio hupunguza shinikizo la damu, lakini pia hukuunganisha na mtu unayemkumbatia. Mgusano wa kimwili unapaswa kuwa zaidi ya tendo la ndoa. Kwa kukumbatiana kila siku, nyote mtaweza kujihisi kuwa mnathaminiwa na kupendwa.