Boss Wangu Ananitaka Kingono, Nipo Njia Panda Naomba Ushauri

Katika harakati za kutafuta kazi nilibahatika kufika ofisi moja maeneo ya Mwenge (Dar es salaam) kwangu ilikua faraja kubwa sababu kiukweli nilikua nahangaika sana na hali ya ugumu wa maisha na sikutaka kabisa kuwa tegemezi kwa mtu yoyote (wakiwemo wazazi) niliamini kunipa elimu ni mtaji muhimu na tosha na lilikua jukumu langu kuandaa maisha yangu mwenyewe na kujitegema

Nilipofika pale niliomba kuonana na boss ila nikaambiwa haiwezekani labda ningekua na appointment, kutokana na uzoefu hii kauli nilikua nimekutana nayo mara kadhaa hivyo ilikua hainisumbui sana, nikamwambia yule receiptionist kuwa nilikua na appointment (kiukweli sikua nayo na nakiri nilidanganya na nilikosea ila sikuwa na namna mbadala) akaniuliza nimwambie we ni nani nikasema mwambie (tax consultant)

Waliongea mawili matatu then nikaruhusiwa kuingia nadiriki kusema shida ni mwalimu mkubwa sana kwani sikuwa na woga wowote kuonana na yeyote na kujinadi, baada ya mazungumzo na mahojiano ya kama dakika sita yule manager (mwanamke) akaniambia alhamisi niende nikafanye interview na kutokana na intro niliyoitoa hiyo siku (Jumanne).

Haikua kazi kwangu kupata hiyo kazi hata baada ya interview ya alhamisi, tulikubaliana terms za kazi na mshahara then nikapewa mkataba. Nilifurahi sana nikijua sasa mipango yangu itaenda vema (kwakweli mshahara ulikua mzuri tu) hadi nikaanza kupangilia biashara ndogondogo ili kuinua uchumi wangu.

Nilianza kazi wiki iliyofuata na wafanyakazi wenzangu walikua watu wema sana kwangu hivyo nilifanya kazi kwa furaha na ufanisi sana mpaka hali ilipokuja kubadilika.

MABADILIKO

Baada ya wiki moja mambo yalianza kubadilika pale ofisini, mara kwa mara boss alikua na vikao visivyokua na mbele wala nyuma na mimi na akawa mkali kwa wafanyakazi wenzangu especially wa kike na taratibu wakaanza kuniogopa.

Siku moja aliniita ofisini (ilikua Ijumaa) na akaniambia nifunge mlango nilishtuka sababu normally ukiingia ofisini lazima ufunge mlango cha kushangaza akaniambia ni-u lock nikafanya alivyotaka,

Hakuna cha maana alichoniambia zaidi ya story za kifamilia tu oooh mara mumewe (aliekuwa meneja kabla hajaumwa) anasumbuliwa na kisukari na presha na anapata taabu sana mi nikawa msikilizaji tu na aliongea muda mrefu hadi jua likazama na watu waliondoka ofisini alibaki mlinzi tu.

Aliongea mengi na mwisho akaniambia anataka nimsaidie (ngono) kitu ambacho kilinishtua kidogo ukizingatia ni mtu mzima rika la mamaangu, nilimbembeleza kuwa hapo si pahali salama ili tu aniache siku hiyo ili nikajipange jinsi ya kuepukana nae na kuikabili ile hali.

Alinikomalia sana hadi kunivamia physically na alionekana wazi alikua desperate for sex ila nilifanikiwa kumpanga na akanielewa baada ya hiyo siku ofisi nzima wakahisi nilizini na yule boss hivyo kukawa na minong'ono mingi na sikuwa na namna ya kuwaaminisha vinginevyo.

Tangu hapo ni wiki ya pili sasa huyu mama ananisumbua sana, ananiahidi mambo mengi kama nitakubali kusex nae na ni dhahiri nikimtamkia kuwa SITAKI nitapoteza kibarua kwani ye ndo meneja hapa na ndo anaajiri na kusitisha ajira,

Leo hii (Jmosi) kanipigia simu na kuniambia kesho saa saba ana kikao na mimi cha kikazi ila location naona hata aibu kuisema. Wakuu najua kuna watu humu wakike na kiume ambao wamekutana na hali kama yangu,

Naipenda kazi na sina pa kushikilia kwa sasa lakini pia sitaki kuisaliti imani yangu na msimamo kwa kupenda vitu vya dezo na kufanya uzinzi na mtu wa rika la mama yangu, ni dhambi kubwa na pia ni kinyume cha maadili ya jamii yetu lakini pia nikifikiria matokeo ya kuachishwa kazi (na mipango niliyokwisha iweka kichwani kwangu) roho inaniuma sana nabaki nikiwaza na kuwazua bila kujua haswaa nishike wapi.

Msimamo wangu ni kutokulala na huyu mama no matter the consequences ila naomba mnipe chakula cha akili ili akinifukuza kazi basi niwe nimeimarika kisaikolojia kwa ushauri wenu na nisitetereke sana kisaikolojia.

Asanteni