Dondoo za kubeti mechi zote za Ligi Kuu Uingereza Jumamosi



Chelsea vs Tottenham Hotspur

Vita kuu na mechi kubwa ya London itapigwa katika uwanja wa Stamford Bridge Jumamosi jioni Chelsea watakapoikaribisha Tottenham Hotspur. Chelsea watakuwa na tumaini kubwa kushinda mechi hii kuendelea kuongoza kileleni mwa msimamo wa ligi. Pia Tottenham wanahitaji kushinda mechi hii kupunguza pengo kati yao na Chelsea hadi pointi moja.

Jumla ya mechi 137 zilizochezwa baina ya Chelsea na Tottenham Hotspur, Chelsea wameshinda mara 58 wakati Spurs wameshinda mechi 44 na mechi 35 zikiwa sare.

Uwezo na kiwango kikubwa cha Chelsea ikilinganishwa na Spurs, vinaweza kuiwezesha Blues kuondoka kifua mbele katika mechi hiyo ya Jumamosi.

Conte ameunda Chelsea ambayo imekuwa hatari zaidi katika wiki zilizopita na tunatarajia kuona kiwango cha juu na soka la kuvutia wikiendi hii.

Ubashiri: Chelsea itashinda kwa wastani wa mabao 2.5 dhidi ya Spurs.

Burnley vs Manchester City

Imeonekana mara kadhaa kuwa Manchester City wamepungukiwa kile kiwango chao bora. Na hawana ushawishi mkubwa wanapokuwa ugenini. Hii ilidhihiri katika sare ya 1-1 waliyopata dhidi ya Monchengladbach katikati ya wiki mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Uefa.

Burnley ni timu iliyopanda daraja, lakini wamekuwa na rekodi nzuri mechi za nyumbani msimu huu. Wamefungwa mara mbili tu katika mechi zao saba, zote kwa goli 1-0. Hivyo tunataraji Burnley watampa wakati mgumu Pep Guardiola na timu yake.

Hata hivyo City wana nafasi kubwa ya kushinda ingawa watapata ushindi mwembamba.

Liverpool vs Sunderland

Tukitazama kiwango cha Liverpool cha sasa, kikosi cha David Moyes hakiwezi kuwa na nafasi ya kutwaa pointi mbele yao katika uwanja wa Anfield. Wataendeleza unanga wao wa Sunderland kama kawaida katika mechi hii.

Aidha, rekodi ya Liverpool kucheka na nyavu katika wiki za hivi karibuni imezidi kukua, wamefunga angalau magoli mawili katika mechi 4 kati ya tano za mwisho. Kwa hakika watafunga angalau mabao mawili katika mechi hii.

Leicester City vs Middleborough

Licha ya kiwango kibovu cha Leicester City katika mechi za Ligi, bado wana nafasi kubwa kushinda mechi hii. Tunataraji wataendeleza mwendo wa ushindi dhidi ya Boro. Wakiwa wameshafuzu hatua ya mtoano Ligi ya Mabingwa katikati ya juma hili, bila shaka morali yao itaendelea kuwa juu Ligi ya Uingereza pia.

Ushindi ni jambo la hakika kwa Leicester lakini timu zote zitaona nyavu.

Swansea vs Crystal Palace

Ingawa mechi nyingi baina ya timu hizi mbili zimeishia sare, kwa hakika kutakuwa na mshindi katika mechi hii inayofuata. Timu zote mbili zina shauku ya kushinda kulingana na nafasi zao katika msimamo wa Ligi.

Hii ni fursa kwa yeyote kati ya timu hizi kupata ushindi. Mechi itakuwa ngumu kwa kila timu, lakini timu zote zinaweza kufunga goli katika mchezo huu.

Crystal Palace itashinda kwa wastani wa 1.90, na zote zitafunga kwa wastani wa 1.70