House girl kaniandikia barua ya mapenzi baada ya mke wangu kwenda kwao kujifungua
Wife yuko mkoani kwa ajili ya kujifungua. Tuliamua aende huko kwa kuwa ni uzazi wake wa kwanza na hapa mjini hatuna ndugu wa kuweza kusaidia mambo ya kumkanda, kumpikia na huduma nyingine kwa mama mzazi.
Akiwa anajiandaa kuondoka, tuliletewa kasichana kadogo ka kazi umri miaka 16.
Kwa kweli sina mazoea nako na muda mwingi niwapo home nautumia kufanya kazi zangu za ofisini.
Leo asubuhi nilimwambia mtoto aniandikie orodha ya vitu tunavyohitaji kwa matumizi ya nyumbani.
Muda huu ndio binti kanipa hiyo orodha ili kesho nikafanye shopping.
Nimeipitia list, na nilipoguza ukurasa wa nyuma ndipo nkakutana na hiyo barua ya mapenzi.
Binti kaanza kwa kunisifia, akamaliza kwa kusema yuko tayari kuwa mpenzi wangu, na anasema tufanye iwe siri mke wangu asijue.
Anadai atahakikisha anamheshimu na kumtii mke wangu.
Hapa nilipo nimechanganyikiwa, maana katoto haka ni kadogo sana sijui ujasiri kameuptata wapi?