Ligi ya Mabingwa Ulaya UEFA Dondoo za kubeti mechi zote za leo



Ni vigumu kwa Legia kufanya kile walichofanya kwa Real Madrid dhidi ya BVB, pia mechi nyingine kali ni Monaco vs Spurs na Sevilla dhidi ya Juve

Monaco vs Tottenham: Utabiri

Monaco wapo katika kiwango chao cha juu na wanarejea tena dimbani wakiwa na mwendo wa mechi 6 bila kufungwa wakishinda 4 na sare 2. Ni hatari wanapokuwa mbele ya goli baada ya kufunga mabao 20 wakiruhusu manne tu. Pia wamecheza mechi tatu bila kuruhusu goli. Hakuna shaka watakuwa hatari hasa mechi inapochezwa katika uwanja wao wa nyumbani.

Tottenham bado hawajashinda mechi katika Ufaransa, na wanahitaji ushindi kwa nguvu zote ili waendelee kubaki kwenye michuano.

Kikosi hicho cha Mauricio Pochettino kimetoa sare 6 katika mechi 8 za mwisho na pia sare 3 katika mechi nne ugenini dhidi ya timu za Ufaransa. Bila shaka tunakwenda kushuhudia sare ya 1-1 hadi filimbi ya mwisho itakapopigwa.

Leicester City vs Club Brugge: Utabiri

Leicester wanaonekana kuelekeza macho yao yote kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa, wamekuwa katika kiwango cha kupaa. Ni mechi ya Leicester na tunatarajia watashinda nyumbani katika mchezo huu. Hata hivyo, hatutaona magoli mengi katika mechi hii, yaweza kuwa goli moja au mawili lakini tunatarajia kwa upande timu ya Ranieri goli hata moja halitaruhusiwa.

Brugger wamecheza mechi 23 dhidi ya timu za Uingereza, mechi 10 zimechezwa katika ardhi ya Uingereza, wamepoteza mechi 13 na kushinda 6.

Sevilla vs Juventus: Utabiri

Mechi ya kwanza katika Italia iliishia kwa sare ingawa Juventus walionekana kupewa nafasi zaidi. Wakati huu, kutakuwa na magoli katika mechi hii kwani timu zote zimelenga kumaliza kileleni mwa kundi. Zote zinatarajiwa kufunga katika mchezo huu kulingana na kiwango chao katika mechi za hivi karibuni.

Timu hizi zimekutana mara tatu katika historia kila moja ikishinda mechi moja na sare moja.

Borussia Dortmund vs Legia Warsaw: Utabiri

Ni vigumu kuamini kwamba Legia wataweza kucheza katika kiwango bomba kama kile walichoonesha dhidi ya Real Madrid. Dortmund ni timu inayojiamini na itakuwa vigumu kuruhusu pointi zichukuliwe katika uwanja wao wa nyumbani.



Hatutarajii muujiza wowote Jumanne kwani Dortmund wanatamani sana kushinda ili kujipanga vizuri kwa mechi nyingine dhidi ya Real Madrid. Tunaweza kutarajia magoli ya kutosha tena, na kuna uwezekano mkubwa klabu hiyo ya Bundesliga ikaongoza kipindi cha kwanza.