PAUL MAKONDA AKATAA KUHONGWA MILIONI 50 KUTOKA KWA MAAJENTI WA SHETANI

Kuna kikundi cha watu 10 walikuja kwangu, ambao nawatambua kama “maajenti wa shetani” ambao wanapata faida kati ya Sh milioni 35 mpaka Sh milioni 45 kwa mwezi kutokana na dawa hizo za kulevya.

Walipanga mikakati ya kunishawishi kupokea Sh milioni tano kwa kila mmoja kwa mwezi yaani Sh milioni 50 ili nisipige kelele kuhusu shisha na wao waendelee kupata faida. “Shisha imerudi katika Mkoa wa Dar es Salaam na nimeshamuagiza Kamishna Sirro, lakini nimeona kama ana kigugumizi… lakini sijajua kama hizi tano tano zimepita kwake na pia RPC wa Kinondoni nimemuona hapa, lakini hawa wana kigugumizi sijui kama hizi tano tano zimepita kwao,” alisema Makonda."