TFF yamfungia kocha wa Yanga Hans van Pluijm mechi 3 na kumpiga faini



Shirikisho la soka Tanzania TFF leo November 22 2016 kupitia kwa kamati ya saa 72 imetangaza kumuadhibu kocha mkuu wa Yanga Hans van Pluijm kwa tuhuma za kuwatolea lugha chafu waamuzi wa mechi.

Kamati ya saa 72 imemfungia kocha Hans van Pluijm mechi tatu kukaa katika benchi na kumpiga faini ya Tsh 500,000 kwa kosa hilo, Hans anatajwa kuwatolewa lugha chafu waamuzi wakati wa mchezo na baada ya mchezo kuwafuata katika vyumba vya kubadilishia nguo.

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Hans van Pluijm alioneshwa kadi nyekundu kwa mara ya kwanza katika maisha yake ya soka kama mchezaji na kama kocha November 10 2016 katika mchezo dhidi ya Ruvu Shooting kwa tuhuma za kupishana kauli na refa.